Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene
akizungumza katika mkutano na waandishi wa Habari uliofanyika leo katika Ukumbi
wa wizara, jijini Dodoma, ambapo ameahidi kuwashughulikia watendaji wa Mamlaka
ya Vitambulisho vya Taifa(Nida) wasiotoa huduma stahiki kwa wananchi wanaofika
kuomba vitambulisho. Picha na Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene akiteta
jambo na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida), Dkt.
Anold Kihaule (kulia) wakati wa Mkutano
na Waandishi wa Habari uliofanyika leo katika Ukumbi wa wizara, jijini Dodoma, ambapo
ameahidi kuwashughulikia watendaji wasiotoa huduma stahiki kwa wananchi
wanaofika kuomba vitambulisho.
Na Mwandishi Wetu, Dodoma
Serikali
imesema mashine chakavu ndio chanzo cha ucheleweshaji wa vitambulisho
vya NIDA kwa wananchi wake hapa nchini, na badala yake wamenunua mashine
mpya yenye thamani ya sh bilion 8.5 yenye uwezo wa kufyatua
vitambulisho 9000 kwa saa.
Mpaka
sasa tayari NIDA imefanikiwa kutoa vitambulisho milioni sita na
kutambua wananchi milioni 21. 8, hadi sasa kati ya watu 27. 7
waliotarajiwa kusajiliwa.
Jumla ya namba za kipekee za utambulisho ni milioni 17. 8 zilikiwa zimezalishwa na zinaweza kutumika katika utambuzi wa watu.
Akizungumza
na waandishi wa habari Waziri wa Mambo ya Ndani George Simbachawene
alisema tayari serikali imenunua mashine mpya ambazo zitakamilishwa
kufungwa April mwaka huu kwa ajili ya kuanza kufanya kazi.
Alisema
mtambo huo mpya una uwezo wa kuzalisha vitambulisho 9, 000 kwa saa
jambo ambalo kwa siku nzima wanauwezo wa kutoa vitambulisho vya kutosha
kwa wananchi wake.
Alisema
mitambo mipya na ikishirikiana na ile ya zamani wanaamini watatoa
vitambulisho vingi ambapo wanatarajia kukamikisha zoezi hilo ndani ya
miaka miwili.
"Safarii
hii vitambulisho vitakuwa bora awali vilivyotolewa havikuwa na ubora
kutokana na mashine kuwa chakavu, " alisema Simbachawene.
Alisema
awali mtambo ulikiwa ukizalisha vitambulisho 500 lakini hivi sass
vitaboreshwa na kuzalishwa vitambulisho vingi kwa siku ili kukamilisha
zoezi hilo.
Hata hivyo
aliwaomba radhi wananchi kutokana na kupata shida katika zoezi hilo
hivyo amewaahidi hivi sasa litafanyika kwa haraka zaidi.
Alisema
mashine hizo ni bora na zitafanikiwa kukamikisha zoezi hilo ndani ya
miaka miwili kwa watanzania wote au pungufu ya miaka hiyo.
Alisema
serikali ilivyojipanga kutekeleza zoezi hilo mamlaka imeendelea na
ukamilishaji wa ufungaji mashine wa mitambo ya kisasa yenye uwezo mkubwa
wa kuzalisha vitambulisho 9, 000 kwa saa moja na zoezi la uzalishaji
vitambulisho litaanza mwishoni mwa Aprili.
Nida
kwa kushirikiana na Idara ya Uhamiaji Kamati za Ulinzi na usalama Idara
ya wakimbizi na Mamlaka ya Mawasiliano nchini TCRA.
Waziri Simbachawene alisema kutokana na utendaji usioridhisha wanatarajia kufanya mabadiliko ndani ya NIDA ili kuboresha.
Alisema pia watakuwa makini katika ugawaji wa vitambulisho kwa wageni wakaazi na wakimbizi.
Zoezi
la utoaji vitambulisho litaendelea ambapo hadi sasa ni watu milioni
sita pekee ndio wamekabidhiwa vitambulisho vya taifa kati ya milioni 27.
7 waliotarajiwa kusajiliwa
No comments:
Post a Comment