WAZIRI
wa Maji,Profesa Makame Mbarawa akizungumza mara baada ya kupokea
taarifa ya utekelezaji wa miradi ya maji wakati wa ziara yake ya siku
tatu mkoani Tanga iliyoanza leo kushoto ni Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji
Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi Geofrey
Hilly.
Mkurugenzi
wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga
Uwasa) Mhandisi Geofrey Hilly akizungumza wakati wa ziara hiyo kushoto
ni Meneja wa Ruwasa Mkoa wa Tanga Mhandisi Upendo Lugongo.
WAZIRI
wa Maji,Profesa Makame Mbarawa kulia akinawa mikono kabla ya kuingia
kwenye ukumbi wa mamlaka ya maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini
Tanga (Tanga Uwasa) wakati wa ziara yake.
WAZIRI wa Maji,Profesa Makame Mbarawa kushoto akisisitiza jambo kwa Mkurugenzi Mamlaka
ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi
Geofrey Hillywakati wa ziara yake mara baada ya kutembelea chanzo cha
maji eneo la Horohoro wilayani Mkinga katikati ni Meneja wa Ruwasa Mkoa wa Tanga Mhandisi Upendo Lugongo.
WAZIRI wa Maji,Profesa Makame Mbarawa kulia akiwa na
Mkurugenzi Mamlaka
ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi
Geofrey Hilly wakati akitoka kutembelea miradi wa maji eneo la Horohoro.
WAZIRI wa Maji,Profesa Makame Mbarawa akitoka kutembelea miradi wa maji eneo la Horohoro.
WAZIRI wa Maji, Profesa Makame Mbarawa,
amemuondoa kwenye nafasi yake aliyekuwa Mkuu wa Kitengo cha Menejimenti ya Manunuzi wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa
Mazingira jijini Tanga(Tanga UWASA)Jamal Ngereja kwa kushindwa kufanya taratibu
za manunuzi ya mabomba na vifaa katika miradi saba ya maji katika wilaya nne
mkoani Tanga inayotekelezwa na Mamlaka hiyo.
Pia Profesa
Mbarawa amefanya maamuzi hayo katika Mamlaka za Maji Safi na Usafi wa Mazingira
za Moshi,Babati na Arusha nakuahidi kuendelea kufanya mabadiliko katika mamlaka nyingine za maji za
Morogoro,Mwanza,
Tabora,Shinyanga na Kahama.
Profesa
Mbarawa amefikia uamuzi huo baada ya Wizara ya Maji kutoa fedha takribani
Sh.Milioni 700 katika miradi saba ya maji katika wilaya za
Pangani,Mkinga,Muheza na Handeni kwa ajili ya ununuzi wa mabomba tangu mwezi
Novemba mwaka jana lakini hakuna chochote kilichofanyika.
Pamoja na kufanya maamuzi hayo lakini pia aliwaonya wahasibu katika
mamlaka za maji nchini nao wajiandae iwapo tu watafanya uzembe katika matumizi ya fedha za miradi ya
maji .“Haiwezekani
tumetoa fedha za utekelezaji wa miradi ya maji katika mikoa ya Mbeya,Iringa na
Tanga kiasi hicho hicho cha fedha lakini wenzenu wamefikia asilimia 70 ya
utekelezaji lakini Tanga hakuna
kilichofanyika,”alisema.
Aliongeza,
“ kutokana na hilo nakuambia kabisa wewe(Afisa Manunuzi) nakuondoa hapa na hili
nitafanya pia kwenye mamlaka za Maji
Safi na Usafi wa Mazingira za Morogoro,Mwanza,Kahama,Shinyanga na Tabora kama nilivyofanya Babati,Moshi na Arusha,”alisema.
Aidha,
kwa upande wa miradi ya maji ambayo haiendi vizuri haswa ya mabwawa, Profesa
Mbarawa, aliahidi kuhakikisha anapeleka wataalamu kutoka wizarani kuchunguza
miradi hiyo kila kitu ilikujua kama inakwenda na thamani ya fedha zilizotumika.
“Nitahakikisha
kuwa ndani ya wiki kwenye miradi ya maji ambayo haiendi vizuri tunaleta
wataalamu kuja kuchunguza kila item(kitu)
kuanzia tofali,urefu wa kibanda,kina cha mabwawa kuona kama inakwenda na value
for money (thamani ya fedha),kutokana tumegundua kuna watu kuanzia ngazi ya
Halmashauri hadi Wizarani walihusika na
hujuma za miradi ya maji kwa kupandisha gharama,”alisema.
Aliongeza, “Nataka nimiambie wakandarasi na
watumishi wa Wizara ambao wamehusika na
huo mchezo mchafu wajiandae safari hii hatuna mchezo”.
Katika
hatua nyingine,Waziri Mbarawa amesema kuwa katika mwaka wa fedha
2020/21,Serikali kupitia Wizara ya Maji imetenga fedha kwa ajili ya kutoa maji
katika chanzo cha mto Zigi hadi katika mjiwa Horohoro wilayani Mkinga wenye
urefu wa kilometa 40.
Amesema
kuwa,mradi huo utavinufaisha vijiji zaidi ya 30 vitakavyopitiwa na mradi huo na
kuahidi pia kuleta wataalamu wa Wakala wa Uchimbaji Visima na Ujenzi(DDCA) kuja
kuchunguza na kufanya tathminikatika bwawa la maji la Horohoro.
No comments:
Post a Comment