Mkuu
wa Mkoa wa Shinyanga Bi. Zainabu Tellack akiongea na wafanyibiashara wa mnada
wa mifugo wa Muhunze ulioko Wilayani Kishapu jana alipofika katika mnada huo
kujionea namna bora ya uzingatiaji wa maelekezo ya Serikali kuhusu kujikinga na
mlipuko wa ugonjwa wa Corona.
PICS4.
Mkuu
wa Mkoa wa Shinyanga Bi. Zainabu Tellack akionesha mfano wa namna bora ya
kunawa wa Mikono kabla ya kuanza ukaguzi wa Kituo cha Afya Kishapu
kitachotumika kuhudumia wagonjwa Corana kama atatokea mgonjwa wa ugonjwa huo
Wilayani Kishapu jana alipofika katika kituo hicho kujionea namna bora ya uzingatiaji wa
maelekezo ya Serikali kuhusu kujikinga na mlipuko wa ugonjwa wa Corona.
Na
Anthony Ishengoma- Sinyanga
Mkuu wa Mkoa wa
Shinyanga Bi. Zainabu Tellack amewataka wazazi na walezi mkoani Shinyanga
kutowaruhusu watoto wadogo kwenda katika mikusanyiko hususani minada ya mazao
na mifugo kama hatua muhimu ya kuwakinga na maambukizi ya ugonjwa wa corona.
Mkuu wa Mkoa
ameyasema hayo wakati alipotembelea mnada wa mifugo wa Muhunze ulioko katika
Makao Makuu ya Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga kwa lengo la kujionea
utekelezaji wa agizo la serikali linalowataka wananchi kuchukua tahadhari ya
kujikinga na ugonjwa wa corona ikiwemo
kuweka maji na sabuni katika maeneo yanayokutanisha watu wengi pamoja na
kukaa umbali wa mita moja.
Bi. Tellack ameonya
kuwa huu si wakati wazazi kutembea na watoto wao kutokana na uwepo wa mlipuko
wa ugonjwa wa Corona na kuwataka kusubiri mpaka wakati ugonjwa huu utakapokuwa
umedhibitiwa kwani uwezo wa watoto kujikinga ni mdogo sana.
Pamoja na agizo hilo
la Mkuu wa Mkoa kwa wakazi na wafanyabiashara katika minada ya mifugo pia
hakuridhishwa na hatua za zuinazochukuliwa na uongozi wa mnada huo za
kuhakikisha wale wote wanaoingia mnadani hapo wanasafisha mikono yao baada ya
kujionea mnada huo ukiwa na njia zaidi ya moja ya kuingia mnadani hapo na kutoa
nafasi kwa baadhi ya watu kujipenyeza ndani ya eneo hilo bila kuchukua
tahadhari ya kujikinga na Corona.
Bi. Tellack amewataka
wafanyabiashara mnadani hapo kuhakikisha wanajikinga na maambukizi hayo kwa
kila mmoja kunawa mikono yake kila mara na kuhakikisha wanakuwa na vitakasa
mikono (sanitizers) kwa vile wanao uwezo wa kuvinunua kama hatua muhimu ya
kujikinga na hatari ya maambukizi hayo.
‘’Nunueni vitakasa
mikono kwa ajili ya usalama wenu kwa sababu hamuwezi kukosa fedha ya kununua ya
kiasi cha shilingo elfu nne na miatano na hata kama ni shilingi elfu kumi kwa
ajili ya kujikinga na kuwakinga wengine.’’Aliendelea kusema kiongozi huyo wa
Mkoa.
Agizo kama hili pia
lilitolewa na Mkuu wa Mkoa kwa wafanyabiashara ndogo wanaofika eneo la mnada
kwa lengo la kujipatia kipato tofauti na mifugo inayouzwa mnadani kuhakikisha
wanakuwa na maji na sabuni vinginevyo watozwe faini kwa kushindwa kutekeleza
agizo hilo muhimu la Serikali.
Pamoja na kutembelea
mnada huo Bi. Tellack pia alitembelea Kituo cha Afya cha Wilaya ya Kishapu
kilichoandaliwa kama sehemu maalumu ya kupeleka wagonjwa wa corona endapo
watabainika Wilayani humo kama hatua muhimu ya kujionea ni namnagani Wilaya ya
Kishapu imejipanga kukabiliana na ugonjwa huo.
Akiwa katika kituo
hicho cha Afya Mkuu wa Mkoa amejionea vifaa vnitakovyotumiwa na waudumu wa Afya
kujikinga na kuwahudumia wagonjwa na kuwataka wahudumu hao kuwa tayari kwa
lengo la kukabiliana na kuhudumia wagonjwa hao kwa tahadhari kubwa.
Mnada huo
unaowakutanisha wafanyabiashara wa mifugo kutoka sehemu mbalimbali za mkoa wa
Shinyanga na mikoa jilani ufanyika kila Siku ya Alhamisi na kuvuta
wafanyabiashara wa aina nyingine nje na ndani ya mnada huo ambao pia wametakiwa
kuchukua tahadhari kwa kuweka vitakasa mikono katika maeneo yao ya biashara.
No comments:
Post a Comment