Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mary Makondo
akizungumza wakati wa kufunga mafunzo kwa watendaji wa sekta ya Ardhi wa ofisi
za Ardhi za mikoa ya Morogoro, Dodoma, Singida na Manyara yaliyofanyika ofisi
za Wizara katika Mji wa Serikali eneo la Mtumba jijini Dodoma.
Kamishna wa Ardhi nchini Nathaniel Nhonge akizungumza wakati wa kufunga mafunzo
ya Watendaji wa sekta ya ardhi wa ofisi za Ardhi za mikoa ya Morogoro, Dodoma,
Singida na Manyara yaliyofanyika ofisi za Wizara katika Mji wa Serikali eneo la
Mtumba jijini Dodoma. (Picha na Wizara ya Ardhi).
Na Munir Shemweta, WANMM DODOMA
Katibu Mkuu Wizara ya
Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mary Makondo amewataka watendaji wa sekta
ya ardhi katika ofisi za mikoa kuepuka urasimu na kufanya kazi kwa kuzingatia
sheria ili kutoa huduma bora na zenye tija kwa wananchi.
Alisema, pamoja na
kutenda kazi kwa kuzingatia sheria, watendaji hao pia wanapaswa kuhakikisha
wanashughulikia kero za wananchi kwa kukaa nao pamoja hasa pale wananchi wanapokosea
kwa lengo la kuwasaidia badala ya kuwakatisha tamaa.
‘’Urasimu uishe, lengo
hapa ni kumhudumia mwananchi na cha msingi ni kukaa pamoja na mteja na kumueleza
alipokesea badala ya kumkatisha tamaa kwa kumzungusha, tuwaonee huruma na
kuacha urasimu usio wa lazima’’. Alisema Mary.
Akizungumza wakati wa
kufunga mafunzo ya Maofisa wa sekta ya ardhi katika mikoa ya Morogoro, Manyara,
Singida na Dodoma katika ofisi za Wizara zilizopo Mji wa Serikali Mtumba jijini
Dodoma jana, Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mary
Makondo aliwataka watendaji hao kuwa wabunifu na kutenda kazi kwa kasi na kusisitiza
kuwa kazi katika maeneo wanayotoka ni nyingi na zinahitaji kushughulikiwa.
Kwa mujibu wa Mary
Makondo, watendaji hao ambao ni Makamishna na Wasajili Wasaidizi wa ofisi za
ardhi za mikoa wahakikishe wanatoa kipaumbele katika kushughulikia migogoro ya
ardhi kwa haraka pamoja na kutilia mkazo mafunzo ya ndani kwa watumishi.
Aidha, alihimiza utoaji
huduma nzuri kwa wateja wanaokwenda kupata huduma katika ofisi za mikoa na
kubainisha kuwa suala hilo linahitaji uvumilivu mkubwa na wakati mwingine kushirikisha
wataalamu wengine wa ofisi moja ili kuja
na uamuzi utakaohusisha mawazo ya wengi.
Akigeukia utoaji hati
za ardhi, Mary Makondo aliwataka watendaji hao kuhakikisha wanaongeza idadi ya utoaji
hati miliki za ardhi kwenye maeneo yao zikiwemo hati za kimila, urasimishaji na leseni za makazi sambamba na kuhakikisha
fidia zinalipwa kwa wakati hususan maeneo yaliyotwaliwa kwa shughuli
mbalimbali.
Vile vile, katibu Mkuu Wizara
ya Ardhi aliwataka watendaji hao wa sekta ya ardhi kuhakikisha wanapata taarifa
zote za makampuni ya urasimishaji na mikataba yao na wakati huo makampuni hayo kufuata
miongozo ikiwemo bei elekezi ya urasimishaji.
Mthamini Mkuu wa
Serikali Evelyne Mugasha alieleza kuwa mafunzo hayo ya watendaji wa sekta ya
ardhi kutoka ofisi za mikoa ya Morogoro, Dodoma, Singida na Manyara yatawawezesha
watendaji wa ardhi wa mikoa kufanya kazi kwa ufanisi kutokana na aina ya mafunzo waliyoyapata
ikiwemo namna ya kuongeza mapato ya serikali kupitia kodi ya ardhi.
Alisema, watendaji hao
walipatiwa mafunzo katika masuala ya ukusanyaji kodi ya pango la ardhi, upimaji
na ramani, mipango miji sambamba na masuala ya maendeleo ya makazi aliyoyaeleza
kuwa watakuwa wakikutana nayo katika utendahji wa kazi za kila
siku.
------------------------------ -----MWISHO------------------- ------------------------------ -----
CAPTION
PICHA
PIX NO
1-
PIX
NO 3- Mthamini Mkuu wa Serikali Evelyne Mugasha
akizungumza wakati wa kufunga mafunzo ya Watendaji wa sekta ya ardhi wa ofisi
za Ardhi za mikoa ya Morogoro, Dodoma, Singida na Manyara yaliyofanyika ofisi
za Wizara katika Mji wa Serikali eneo la Mtumba jijini Dodoma jana.
PIX
NO 4-
Watendaji wa sekta ya Ardhi wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi Nyumba
na Maendeleo ya Makazi Mary Makondo (Hayupo pichani) wakati wa kufunga mafunzo
kwa Watendaji wa sekta ya ardhi wa ofisi
za Ardhi za mikoa ya Morogoro, Dodoma, Singida na Manyara yaliyofanyika ofisi
za Wizara katika Mji wa Serikali eneo la Mtumba jijini Dodoma jana (PICHA ZOTE NA MUNIR SHEMWETA).
No comments:
Post a Comment