HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 16, 2020

PROFESA KIKULA AONGOZA KIKAO CHA TUME YA MADINI

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula ameongoza kikao cha kazi cha Tume ya Madini kilichofanyika jijini Dodoma lengo likiwa ni kupokea na kujadili taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Tume kwa kipindi cha robo mwaka.

Kikao hicho kimeshirikisha Makamishna wa Tume ya Madini ambao ni pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mary Makondo, Katibu Mkuu wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Faraji Mnyepe na Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dkt. Evaristo Longopa.

Makamishna wengine ni pamoja na Mtendaji Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wachimbaji wa Madini Tanzania (FEMATA), Haroun Kinega, Prof. Abdulkarim Mruma na Dkt. Athanas Macheyeki. 
 








No comments:

Post a Comment

Pages