*Sherehe za Muungano,
Mei Mosi zaahirishwa
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza, kwenye kikao cha Kamati ya
Kitaifa ya Uratibu wa Mapambano dhidi ya Ugonjwa wa Homa kali ya Mapafu
(COVID - 19), kilichofanyika katika, ukumbi wa Hazina, jijini Dodoma,
Aprili 14, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, kwenye kikao
cha Kamati ya Kitaifa ya Uratibu wa Mapambano dhidi ya Ugonjwa wa Homa
kali ya Mapafu (COVID - 19), kilichofanyika katika, ukumbi wa Hazina,
jijini Dodoma, Aprili 14, 2020. ( Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri wa Afya Zanzibar, Hamad Rashid, akizungumza jambo, kwenye kikao
cha Kamati ya Kitaifa ya Uratibu wa Mapambano dhidi ya Ugonjwa wa Homa
kali ya Mapafu (COVID - 19), kilichofanyika katika, ukumbi wa Hazina,
jijini Dodoma, Aprili 14, 2020. ( Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy
Mwalimu, akizungumza jambo, kwenye kikao cha Kamati ya Kitaifa ya
Uratibu wa Mapambano dhidi ya Ugonjwa wa Homa kali ya Mapafu (COVID -
19), kilichofanyika katika, ukumbi wa Hazina, jijini Dodoma, Aprili 14,
2020. ( Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Dodoma, Tanzania
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema
agizo la kufungwa kwa shule za awali, msingi, sekondari na vyuo
vyote vya elimu ya kati na vya elimu ya juu litaendelea kubaki vile vile hadi
hapo Serikali itakapotoa tamko jingine.
Pia,
Waziri Mkuu amesema Rais Dkt. John Pombe Magufuli amesitisha maadhimisho ya
Sherehe za Muungano (Aprili 26) pamoja na Sikukuu ya Wafanyakazi (Mei Mosi) ili
kuepuka msongamano na kuendelea kuzuia virusi vya corona visisambae zaidi.
Waziri
Mkuu ameyasema hayo leo (Jumanne, Aprili 14, 2020) katika kikao cha Kamati ya
Kitaifa ya Uratibu wa Mapambano Dhidi ya ugonjwa
wa Homa ya Mapafu unaotokana na maambukizi ya Virusi vya Corona (COVID-19). Amesema
hadi leo, nchini kuna jumla ya watu 53 waliobainika kuwa na virusi vya corona
ikiwa ni ongezeko la wagonjwa wanne ambao wote wapo jijini Dar es Salaam.
Amesema
Serikali bado haijatangaza kuhusu kufunguliwa kwa shule, vyuo na shughuli za
michezo pamoja na misongamano isiyokuwa ya lazima, hivyo maeneo hayo
yataendelea kusalia katika karantini na wanafunzi wote wandelee kubakia
majumbani kwao.
Hata
hivyo, Waziri Mkuu amesema Rais Dkt. Magufuli ameagiza sh. milioni 500 ambazo
zilitengwa kwa ajili ya maadhimisho ya miaka 56 ya Sherehe za Muungano
zipelekwe kwenye mfuko wa kupambana na COVID-19 wa Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar.
Pia,
Waziri Mkuu amewaomba wadau mbalimbali waendelee kuiunga mkono Serikali katika
mapambano dhidi ya virusi vya corona kwani janga hilo ni kubwa na wanaweza
kutuma fedha kupitia akaunti Na: 9921159801 yenye jina
la National Relief Fund Electronic.
Kadhalika,
Waziri Mkuu amesema elimu ya tahadhari ni muhimu ikaendelea kutolewa kwa
wananchi ili waweze kujikinga na maambukizi ya homa kali ya mapafu
inayosababishwa na virusi vya corona. “Kama si lazima kutoka, wananchi
waendelee kutulia majumbani mwao.”
Amesema
Wakuu wa Mikoa na Wilaya waendelee kusimamia utoaji wa elimu ya kujikinga na
virusi hivyo hasa katika mkoa wa Dar es Salaam ambao unaongoza kwa kuwa na
wagonjwa wengi ikifuatiwa na Zanziba. “Ni muhimu wananchi wake wakapewa
tahadhari juu ya namna ya kijikinga.”
Waziri
Mkuu ameagiza kuwa wataalamu wanaosimamia utoaji wa huduma katika maeneo yaliyotengwa
kwa ajili ya wa watu wenye maambukizi ya COVID-19, wakiwemo madaktari wote
wapewe vifaa vya kijikinga ili kuhakikisha hawapati maambukizi ya ugonjwa huo.
Amesema
watu waliokutana na wagonjwa waendelee kufuatiliwa kwa umakini na wahusika
wawashirikishe viongozi wote hadi wa ngazi za chini na kwamba athari za
kiuchumi zinazojitokeza kufuatia ugonjwa huo ziendelee kuchambuliwa.
Machi
17, 2020 na Machi 18, 2020, Serikali ilitangaza kuzifunga shule za awali,
msingi, sekondari na vyuo vyote vya elimu ya kati na vya elimu ya juu kwa muda wa siku 30 na kwamba
wanafuzi wa kidato cha sita waliopaswa kuanza mitihani Mei 4, 2020 nao wangepaswa
kusubiri Wizara ifanye utaratibu mwingine kulingana na matokeo ya hali ya
maambukizi.
Akitangaza
uamuzi huo, Waziri Mkuu pia alisisitiza kuwa mikusanyiko yote mikubwa ya ndani
na nje isiyo ya lazima imesitishwa ikiwemo shughuli za michezo, matamasha ya
muziki, mikutano mbalimbali ikiwemo ya shughuli za kisiasa, mahafali na
shughuli nyingine za kijamii.
Alizitaka wizara
na taasisi zizitishe semina, warsha, makongamano na mikutano yote hapa nchini
ambayo inahusisha washiriki toka nchi zenye maambukizi makubwa. “Watanzania
wenye safari zisizo za lazima kwenye nchi zenye maambukizi makubwa,
wanashauriwa wasitishe safari hizo,” alisisitiza.
Akielezea
hatua nyingine zilizochukuliwa na Serikali ili kudhibiti ugonjwa huo, Waziri
Mkuu alisema Serikali imesitisha michezo yote inayokusanya makundi ya watu
ikiwemo Ligi Kuu ya Tanzania Bara (VPL), Ligi Daraja la Kwanza (FDL), Ligi
Daraja la Pili (SDL) na aina nyngine.
No comments:
Post a Comment