HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 13, 2020

WAGONJWA WA CORONA WAONGEZEKA ZANZIBAR

Wagonjwa watatu wapya walioambukizwa maradhi ya corona wameripotiwa jana na kufanya jumla ya wagonjwa 12 walioambukizwa maradhi hayo hadi kufikia Aprili mwaka huu.

Kwa mujibu wa Waziri wa Afya Zanzibar, Hamad Rashid Mohamed, wagonjwa wote walioongezeka ni Watanzania na hawana historia ya kusafiri nje ya nchi katika siku za
hivi karibuni.
 
Aliwataja wagonjwa hao kuwa ni wanaume wawili mmoja mkazi wa Mwanakwerekwe na mwingine anatoka Bumbwisudi pamoja na mwanamke mwenye umri wa miaka 22 mkazi wa Jang’ombe.
 
Alieleza kuwa wagonjwa wawili waliokuwa wakipatiwa matibabu katika kituo cha Kidimni wameshapona na kuruhusiwa kurudi nyumbani, huku wakitakiwa
kuendelea kubaki ndani bila ya kuchanganyika na watu wengine kwa muda wa siku 14.

Waziri Hamad alisema wagonjwa wengine wanaendelea kupatiwa matibabu katika kituo maalum cha Kidimni na kile cha Skuli ya JKU Mtoni kilichofunguliwa hivi karibuni
kutokana na kuongezeka kwa idadi ya
wagonjwa.

Waziri huyo alithibitisha kuwa wagonjwa wote waliopo katika vituo hivyo, wanaendelea vizuri na afya zao zinaendelea kuimarika siku hadi siku.
 
Aliwataka wananchi kuchukua tahadhari za ziada na kuzingatia maelekezo yanayotolewa na serikali na wataalamu wa afya ili kuhakikisha wanazuia maambukizi mapya ya corona.

No comments:

Post a Comment

Pages