HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 08, 2020

TANGA BEACH RESORT YAFUNGWA KUKABILIANA NA CORONA

 Meneja  wa Hoteli ya Tanga Beach Resort, Joseph Ngonyo, akizungumza na waandishi wa habari leo kuhusu kufungwa kwa hoteli hiyo ikiwa ni kuunga mkono juhudi za Serikali  kuzuia mikusanyiko.
Muonekano wa Hoteli Tanga Beach Resort.

 MENEJIMENTI  ya uongozi wa hoteli yenye hadhi ya nyota tano ya Tanga Beach resort iliyoko jiji Tanga imelazimika kufunga hotel hiyo ili kuunga mkono jitihada za serikali za kuzuia mikusanyiko ili kujikinga na ugonjwa wa virusi vya Corona vinavyotokisa dunia kwa sasa.

Akitoa tamko hilo mbele ya waandishi wa habari Meneja wa hotel hiyo Joseph Ngonyo alisema kuwa wameamua kufunga kutokana na mlipuko wa ugonjwa huo hapa Tanzania pamoja na na kudhibiti mkusanyiko wa watu

Alisemam kuwa  awali tayari biashara ya hotel ilianza kususasua kutokana na uwepo wa ugonjwa huo hivyo kulazima kufunga ili kuzuia mkusanyiko wa waty hasa katika kipindi hiki cha kuelekea katika msimu wa sikukuu.

“Dunia  sasa hivi na hata nchini kwetu kumekuwa na tatizo la gonjwa la Corona hivyo tumeamua kusitisha huduma ili kuunga mkono kauli ya serikali ya kuzui mkusanyiko wa wau wengi pamoja hivyo ili kuwathibiti tumelazimika kufunga hotel hiyo”alisema Ngonyo.

Aidha aliwataka wananchi kuacha dhana potofu ambazo zimeanza kusambaa katika mitandao ya kijamii na kwamba wameamua kuunga mkono juhudi za serikali hivyo shughuli za hotel zinatarajiwa kuanza tena mwishoni mwa mwezi Mei.

Kwa  upande wake mmoja wa wafanyakazi katika hotel hiyo Hadija Ramadhani alisema kuwa wamelazimika kuunga mkono maagizo ya serikali ili kupunguza  maambukizi kwa wafanyakazi pamoja na wananchi ambao wanaweza kufika katika hotel kwa ajili ya kupata huduma.

“Tunaomba watu waachane  na habari za mitandao kwani zinatuchafua lakini lengo letu ni kuhakikisha usalama wa wafanyakazi wetu pamoja na wateja ambao wanakuja kupata huduma katika hotel yety”alisema Ramadhani

Naye kwa upande wake mfanyakazi wa Hoteli hiyo kitengo cha mapokezi Khadija Mcharo alisema kwa sasa huduma zao wamesitisha kutokana na uwepo wa virusi vya Corona na wanaiunga mkono serikali katika juhudi zake za kupambana kupunguza maambukizi hayo.

No comments:

Post a Comment

Pages