Baadhi ya viongozi wa Dini na waumini wakiwa katika wa
maombi na dua maalumu leo ya kuuweka Mkoa wa Tabora ,Taifa na Dunia
nzima mikononi mwa Mungu ili awakinge na janga la ugonjwa wa Corona.
Mganga
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Dkt. Honoratha Rutatinisibwa akitoa taarifa ya
mikakati ya Mkoa huo katika kudhibiti ugonjwa wa Covid -19 wakati wa
maombi na dua maalumu leo ya Viongozi wa Dini na Serikali ya Mkoa wa
Tabora kwa ajili ya kuuweka Mkoa wa Tabora ,Taifa na Dunia nzima
mikononi mwa Mungu ili awakinge na janga la ugonjwa wa Corona.
Katibu
Tawala Mkoa wa Tabora Msalika Makungu akitoa maelezo leo kuhusu hatua
mbalimbali zilikwishachukuliwa katika kujinga na ugonjwa wa covid -19 wakati
wa maombi na dua maalumu Viongozi wa Dini na Serikali ya Mkoa wa
Tabora kwa ajili ya kuuweka Mkoa wa Tabora ,Taifa na Dunia nzima
mikononi mwa Mungu ili awakinge na janga la ugonjwa wa Corona.
Mkuu
wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri akitoa leo maelezo ya juhudi
zinazoendelea za kuhakikisha Mkoa huo unajikinga na ugonjwa wa Covid
-19 wakati
wa maombi na dua maalumu Viongozi wa Dini na Serikali ya Mkoa wa
Tabora kwa ajili ya kuuweka Mkoa wa Tabora ,Taifa na Dunia nzima
mikononi mwa Mungu ili awakinge na janga la ugonjwa wa Corona.
Askofu Mkuu wa Jimbo kuu la Tabora Mhashamu Paul Ruzoka akitoa
maelezo leo ya hatua ambazo wamezichukua katika kukabiliana na janga la
Corona wakati wa utoaji wa huduma za kiroho. Askofu Ruzoka ametoa kauli
hiyo leo wakati
wa maombi na dua maalumu Viongozi wa Dini na Serikali ya Mkoa wa
Tabora kwa ajili ya kumlilia Mungu auokee Mkoa wa Tabora ,Taifa na Dunia
nzima na janga la ugonjwa wa Corona. Picha na Tiganya Vincent.
Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Tabora Ibrahim Mavembi akitoa
maelezo leo ya hatua ambazo wamezichukua katika kukabiliana na janga la
Corona wakati wa utoaji wa huduma za kiroho. Sheikh Mavumbi ametoa
kauli hiyo leo wakati
wa maombi na dua maalumu Viongozi wa Dini na Serikali ya Mkoa wa
Tabora kwa ajili ya kumuomba Mungu kuwaondolea janga la ugonjwa wa
Corona.
NA TIGANYA VINCENT, TABORA
VIONGOZI wa Dini Mkoani Tabora wameiomba
Serikali kutowaone aibu wale wote wanaoleta mzaha na wanaotafuta umaarufu
kupitia janga la ugonjwa wa homa kali ya mapafu unaoeneza na kirusi
kipya aina ya Corona Covid-19.
Kauli hiyo imetolewa leo wakati wa maombi na dua maalumu Viongozi
wa Dini na Serikali ya Mkoa wa Tabora kwa ajili ya kuuweka Mkoa wa Tabora
,Taifa na Dunia nzima mikononi mwa Mungu ili awakinge na janga la ugonjwa wa
Corona.
Mchungaji wa Kanisa la Agape Miracle Centre Elias Mbagata alisema
bado kuna kuna mizaa inaendelea juu ya janga hili hivyo ameiomba serikali
isiwaonee haya wanoendekeza hayo hata kama ni viongozi wakubwa wakiwemo wa
Dini.
Alisema kinachotakiwa kufanywa kwa sasa ni kuwajengea matumaini
wananchi badala ya kuwajaza hofu ambayo itawasababisha wachanganyikiwe.
Askofu wa wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Tabora, Dk Elias Chakupewa alisema wameshachukua hatua mbalimbali za
kuwaelimisha waumini wao kufuata taratibu zote zinazotakiwa ikiwemo maelekezo
ya wataalamu na viongozi wa Serikali namna sahihi ya kujikinga na janga la
Covid -19.
Askofu Mkuu wa Jimbo kuu
la Tabora Mhashamu Paul Ruzoka aliwaomba waumini kuungana na serikali katika
kupigana vita hii iliyo mbele yao kwa kuhakikisha wanatekeleza maelekezo
yanayotolewa na viongozi pamoja na wataalam wa afya.
Alisema Kanisa hilo limesitisha kwa muda baadhi ya taratibu za
uendesha wa Ibada ikiwa ni seehemu ya mikakati ya kuungana na Serikali katika
mapambano dhidi ya Covid -19.
Kwa upande wa Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Tabora Ibrahim Mavumbi
aliwashauri viongozi wa Dini kuendelea kushirikiana na serikali na kufuata
maelekezo ya wataalamu katika kuhakikisha wananchi na waumini wao wanapata
maelekezo sahihi kwa ajili ya kudhibiti ugonjwa huo hatari.
Askofu wa Kanisa la Morovian Tanzania Magharibi Ezekiel Yona
alisema wao kwa kutambua ukubwa wa tatizo wametoa jingo katika Hospitali yao ya
Sikonge kwa ajili ya kutoa huduma kwa wagonjwa wa Covid -19 kama kwa bahati
mbaya wataonekana.
Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT)
Dayosisi ya Magharibi Kati,
Askofu Isaac Laizer alimpongeza Rais Dokta John Pombe Magufuli
kwa kwa kuthubutu kuitangazia dunia kwamba janga la ugonjwa wa
Corona litamalizika kwa wananchi watakapokubali kumuomba Mungu.
Alisema wao wanaungana na Serikali kwa kusimamisha baadhi ya
huduma ikiwemo ya mafunzo kwa watoto wadogo (Sunday school) na kualika
wataalamu kutoa elimu ya kujikinga na Corona.
Viongozi hao wamadhehebu ya dini wamesema kwamba pamoja na
serikali kuchukua taadhali inabidi wananchi kumlilia Mungu ili awasamehe dhambi
na kuwaepusha na janga hilo.
Kwa upande wa Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri aliwashukuru
viongozi hao wa kiroho kwa ushirikiano wanaotoa kwa Serikali na kuwaomba
wasaidie kufikisha elimu kwa waumini wao ili isaidie kuuepusha Mkoa huo na
janga la Covid 19.
No comments:
Post a Comment