Kaimu Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya
Iringa Joseph Ryata akiwa katika soko la Ipogolo alipofanya Ziara katika masoko ya manispaa ya Iringa kwa lengo la kujua namna gani wafanyabisha wanaelimu ya kupambana na Virusi vya Corona
Kaimu
Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya
Iringa Joseph Ryata akiwa katika soko la Mlandege alipofanya Ziara katika
masoko ya manispaa ya Iringa kwa lengo la kujua namna gani wafanyabisha
wanaelimu ya kupambana na Virusi vya Corona
Kaimu
Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya
Iringa Joseph Ryata akiwa katika soko la Ipogolo alipofanya Ziara katika
masoko ya manispaa ya Iringa kwa lengo la kujua namna gani wafanyabisha
wanaelimu ya kupambana na Virusi vya Corona.
NA FREDY MGUNDA, IRINGA
WAFANYABIASHA soko la Kihesa
Manispaa ya Iringa wameomba kuwepo na Askari wa Jeshi la akiba katika maeneo ya
masoko ili kuwakamata wateja wanaokaidi kwa makusudi agizo la kutakasa mikono
ili kujikinga na virusi vya Corona.
Akizungumza mbele ya kaimu meya
wa Manispaa ya Iringa na wataalamu wa afya waliotembelea sokoni hapo Mwenyekiti
wa soko hilo Subira Mohamedi amesema baadhi ya wateja wanakataa kutumia
vitakasa mikono na kuzua hofu ya maambukizi.
Kaimu Meya wa Manispaa ya
Iringa Joseph Ryata alisema Halmashauri haitosita kuchukua hatua za kisheria
ikiwamo kuwafungulia mashtaka, watakaokaidi maagizo ya Wataalamu wa Afya
yanayolenga kukabiliana na maambikizi ya corona
“Nimesikitishwa na kitendo cha wananchi kukataa kunawa mikono kwa
sababu hiyo serikali itawachukulia hatua za kisheria kukabiriana na wananchi
wanaogoma kutakasa mikono” alisema Ryata
Akiwa katika ziara maalam ya ukaguzi wa mwenendo wa mapamabano ya
kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona katika masoko ya manispaa ya
Iringa Kaimu Meya wa Manispaa ya Iringa Joseph Nzala Ryata alitembelea soko la
kuu jipya la Mlandege,soko la ipogolo na soko la Kihesa, alisema kuwa bado kuna
haja kubwa ya kuwaelimisha wananchi juu ya namna bora zaidi ya kujikinga na
maambukizi ya corona.
“Bado kunatatizo kubwa na wananchi kutokuwa na elimu ya kupambana
na virusi vya Corona katika Manispaa ya Iringa,hivyo kunahaja ya kutoa elimu
endelevu ili wananchi watambue madhara yanayotokana na virusi hivyo” alisema
Ryata
Ryata alisema bado kuna mikusanyiko mikubwa isiozingatia umbali
unaotakiwa na wataalamu wa afya wamesema ni miongoni mwa changamoto yenye hatari
kubwa pindi maambukizi yanapoibuka.
Hata hivyo hali ni tofauti kabisa katika Soko la Kihesa ambalo
wamefanikiwa kuweka maji na sabuni maeneo yote ya kuingia na kutoka sokoni hapo
pamoja na maeneo ya ziada wakiwa na lengo mahususi la kujikinga wao wenyewe
Lakini changamoto inayoibuka
ni baadhi ya wateja kukataa kutakasa mikono yao kutokana na wananchi wengi bado
hawana elimu ya kujikinga na virusi vya Corona.
Kwa Upande wake afisa Afya John Bwire alisema wananchi wote
watakaokaidi kutakasa mikono yao watakabiliwa na adhabu kali kwa mujibu wa
kisheria za nchi
Aidha katika Ziara hiyo Mganga mkuu wa Manispaa ya Iringa Jesca
Leba alisema wanaendelea na mkakati wa kutoa tahadhari na elimu katika maeneo yote
ya mikusanyiko
No comments:
Post a Comment