Mbunge wa Jimbo la Vwawa ambaye ni Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga akizungumza mara baada ya kupewa nafasi wakati wa ibada ya Pasaka katika Kanisa la Last Church lililopo katika Mji Mdogo wa Vwawa Mkoani Songwe leo Aprili 12, 2020. (Picha na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo).
Sehemu ya waumini wa kanisa la Last Church wakifurahia salamu za Mbunge wa Jimbo la Vwawa ambaye ni Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga wakati akizungumza kwenye ibada ya Pasaka katika Kanisa la Last Church lililopo katika Mji Mdogo wa Vwawa Mkoani Songwe.
Mbunge wa Jimbo la Vwawa ambaye ni Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga, akizungumza mara baada ya kupewa nafasi wakati wa Ibada ya Pasaka katika Kanisa la Last Church lililopo katika Mji Mdogo wa Vwawa Mkoani Songwe.
Sehemu ya waumini wa kanisa la Last Church wakimsikiliza Mbunge wa Vwawa ambaye pia ni Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga, wakati akizungumza kwenye Ibada ya Pasaka katika Kanisa la Last Church lililopo katika Mji Mdogo wa Vwawa mkoani Songwe.
Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Songwe
Mbunge wa Jimbo la Vwawa ambaye ni Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga ametoa salamu za pole kwa Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Dkt Ayub Rioba, familia nzima ya televisheni hiyo na wafiwa wote kwa misiba ya wanahabari wake.
Ametoa salamu za pole kwa uongozi wa TBC na wafiwa wote kwa misiba ya hivi karibuni kituoni hapo.
Ametoa salamu hizo mbele ya waumini wa kanisa la Last Church lililopo Mjini Vwawa mkoani Songwe wakati wa ibada ya Pasaka leo tarehe 12 Aprili 2020.
Waziri Hasunga ametumia nafasi hiyo kuwakumbusha viongozi wa dini na waumini wote nchini kujikinga dhidi ya maambukizo ya virusi vya Corona wakati wakiwa katika ibada na kwenye shughuli zao za kila siku.
Waziri Hasunga amewataka watanzania wote kwa pamoja kutambua kuwa ugonjwa huo ni janga la Dunia nzima lisilobagua matajiri wala masiki hivyo muhimu kila mmoja kuchukua tahadhari iwezekanavyo.
Wakristo kote Ulimwenguni leo Aprili 12, 2020 wameungana kusherehekea siku ya kumbukizi ya kufufuka kwa Yesu Kristo maarufu kama Pasaka.
No comments:
Post a Comment