HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

May 24, 2020

ALIYEMUOKOA MTOTO KATIKA SHIMO LA CHOO AAHIDI KUMLEA

Denis Minja.      


Na Lydia lugakila, Kagera
 
Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wilayani Ngara mkoani Kagera, Denis Minja aliyemwokoa mtoto mwenye umri wa mwaka mmoja aliyetelekezwa katika shimo la choo cha Shule ya Msingi Murgwanza wilayani Ngara amepandishwa cheo huku akiahidi kumlea mtoto
huyo.

Askari Denis Minja amepandishwa cheo kipya cha Koplo kutoka cha zamani cha Konstebo na kamanda wa jeshi la
Zimamoto na Uokoaji mkoani Kagera Hamis Dawa ambapo amesema kuwa askari huyo amepandishwa rasmi cheo hicho na Kamishna Jenerali wa jeshi hilo, John Masunga kutokana na ujasiri wake wa kuingia katika shimo la choo na kumwokoa mtoto aliyetelekezwa mnamo mei 21 mwaka huu wilayani Ngara mkoani Kagera.

Akielezea juu ya kumlea mtoto huyo askari Denis Minja amesema kuwa ameishafanya mazungumzo na familia
yake na wamekubaliana kumlea na kuiomba serikali
kumruhusu kulea mtoto huyo.
 
Aidha ameongeza kuwa tayari amefuatilia idara ya ustawi
wa jamii na kuelezwa kuwa baada ya kuruhusiwa kwa

mtoto huyo kutoka katika hospitali ya Ngara atafuata
taratibu zote ili akabidhiwe mtoto huyo.  skari huyo amesema ametumia ujasiri mkubwa kumwokoa mtoto huyo aliposikia sauti yake ndani ya shimo hilo lenye urefu wa mita 30.

Hata hivyo kamanda wa jeshi la zimamoto na uokoaji mkoani kagera Hamis Dawa ameiwataka jamii mkoani kuacha mara moja vitendo vya utelekezaji wa watoto kwani vinaonekana kukithiri mkoani hapa.

No comments:

Post a Comment

Pages