HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

May 18, 2020

Prof. Ndalichako awatahadharisha Bodi ya Mikopo

Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya wanafunzi wa Elimu ya Juu Abdul-Razaq Badru akizunguza wakati  Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako alipofanya ziara leo katika ofisi zao zilizopo eneo la Tazara jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof Joyce Ndalichako, akizungumza na Menejimenti ya Bodi ya Mikopo ya wanafunzi wa elimu ya Juu (hawapo pichani) wakati alipofanya ziara leo Jijini Dar es Salaam.
 
Baadhi ya wajumbe wa Menejimenti ya Bodi ya Mikopo ya wanafunzi wa elimu ya Juu wakimsikiliza Waziri qa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako (hayupo pichani) alipofanya ziara kwenye Bodi hiyo.


Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya wanafunzi wa Elimu ya Juu Abdul-Razaq Badru akimuonesha  Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako maeneo mengine ya ofisi za Bodi wakati alipofanya ziara katika ofisi zao  zilizopo eneo la Tazara jijini Dar es Salaam. 
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako, akiagana na Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu Abdul-Razaq Badru, mara baada ya kuhitimisha ziara yake kwenye ofisi za Bodi zilizopo eneo la Tazara jijini Dar es Salaam.


 

Na Irene Mark

WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako ameitaka Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB) kujiandaa kutoa mikopo wakati wowote Serikali itakapofungua vyuo.

Waziri Ndalichako alisema hayo Dar es Salaam leo Mei 18,2020 alipokagua ofisi mpya za (HESLB) zilizopo Tazara jijini hapa na kusema wakati wowote vyuo vitafunguliwa hivyo lazima wapate fedha hizo kwa wakati.

”Katika kipindi hiki ambapo vyuo vya elimu ya juu vimefungwa, HESLB ihakikishe inatumia muda huu kufanyia kazi changamoto zote za wanafunzi ili vyuo vitakapofunguliwa malipo ya mikopo ya wanafunzi yafanyike kwa wakati,” alisema Waziri Ndalichako.

Pia ameipongeza HESLB kwa kutekeleza agizo la Serikali la Kuhakikisha Taasisi zote za umma zinahamia kwenye majengo ya serikali ili kupunguza gharama uendeshaji wa shughuli zake.

"Hapa sasa naamini mtafanyakazi kwa utulivu na mtaongeza ufanisi," alisisitiza Profesa Ndalichako.

Waziri huyo alitumia fursa hiyo kuwakumbusha watumishi wa HESLB kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya maambukizi ya virusi vya corona.

Akizungumza katika kikao hicho, Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB Abdul-Razaq Badru alisema HESLB ipo tayari kuwahudumia wanafunzi muda wowote vyuo vitakapofunguliwa kwa kuwa fedha zinazohitajika, mifumo na taarifa za wanafunzi zipo.

No comments:

Post a Comment

Pages