Mbunge wa Singida Magharibi, Elibariki Kingu ( kushoto) akikabidhi lisiti ya ununuzi wa mifuko 50 ya saruji kwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya ya Ikungi, Japhari Dude, yenye thamani ya shilingi 800,000 ili kusaidia uanzaji wa ujenzi wa nyumba ya katibu wa umoja huo katika hafla iliyofanyika jana Viwanja vya Ofisi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ikungi. Kulia ni Katibu wa UVCCM wa wilaya hiyo, Himidi Tweve.
Mbunge wa Singida Magharibi, Elibariki Kingu, akisaidia kubeba saruji hiyo kutoka katika dukani na kuipakia kwenye mkokoteni.
Mbunge wa Singida Magharibi, Elibariki Kingu, akisaidia kusukuma mkokoteni wenye saruji hiyo kabla ya kuikabidhi. Kulia ni Katibu wa UVCCM wa wilaya hiyo, Himidi Tweve.
Sehemu ya saruji iliyo kabidhiwa.
Na Dotto Mwaibale, Singida
MBUNGE wa Singida Magharibi, Elibariki Kingu amesaidia mifuko ya saruji 50 yenye thamani ya shilingi 800,000 ili kusaidia kuanza ujenzi wa nyumba ya Katibu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya ya Ikungi.
Elibariki Kingu alikabidhi msaada huo jana kama sehemu ya kuunga mkono juhudi za umoja huo wa kujenga nyumba za makatibu wake ambapo pia hivi karibuni alitoa msaada wa namna hiyo kwa kununua mabati 60 yenye thamani ya shilingi 1,300,000 kwa ajili ya upauaji wa nyumba ya Katibu wa UVCCM Mkoa wa Singida.
"Kutokana na imani niliyo nayo kwa chama changu na UVCCM nimeona ni vema kuwaunga mkono katika ujenzi huu kwa kununua mifuko hii 50 ya saruji ya kuanzia na kama mtaonesha moyo wa kujitoa nitahakikisha ujenzi wa nyumba hiyo unakamilika ndani ya wiki mbili" alisema Kingu.
Akipokea saruji hiyo kwa niaba ya kamati ya utekelezaji ya UVCCM Wilaya ya Ikungi, Mwenyekiti wa UVCCM wa wilaya hiyo, Japhari Dude, alimshukuru mbunge huyo kwa kwa msaada huo na moyo wa kujitoa katika shughuli mbalimbali za chama.
Mbali na msaada huo Kingu alitoa msaada wa viti 20 katika Kanisa la FPCT la Kijiji cha Nkuninkana.
No comments:
Post a Comment