HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

May 10, 2020

DC TANO MWERA AKUTANA NA WACHIMBAJI WADOGO KIJIJI CHA IMALAMATE-BUSEGA

Mkuu wa Wilaya ya Busega, Tano Mwera (katikati), akifanya kikao cha awali na viongozi wa madini pamoja na wawakilishi wa wachimbaji wadogo, katika mgodi wa Imalamate.



Na Mwandishi Wetu, Busega

MKUU wa Wilaya ya Busega, Tano Mwera, ametembelea eneo la Machimbo, Kijiji cha Imalamate  na kufanya kikao na viongozi wa Madini Mkoa wa Simiyu pamoja na Wachimbaji wadogo.

Kikoa hicho chenye lengo la kusikiliza changamoto za wachimbaji wadogo, kutoa maelekezo ya Serikali na kufafanua mkokotoo wa Asilimia za mapato kwa pande zote husika juu ya mapato ya madini.

Pia kuweka mkakati wa kuthibiti utoroshaji wa dhahabu kwenda nje ya nchi ikiwemo nchi jirani ya Kenya.

Awali DC Tano Mwera alibaini changamoto mbalimbali ambazo kwa kiasi kikubwa zinasabishwa na ukosefu wa taarifa sahihi kwa wachimbaji hao ambapo amechukua muda wake kuwaelewesha wachimbaji wadogo juu ya Mkokotoo wa mapato ya Serikali kutokana na waraka wa Serikali wa maeneo yenye mlipuko wa madini (RUSH).

"Mkokotoo huo unaweka wazi mapato ya Serikali kuu ambayo ni Mrahaba na gharama za ukaguzi ambazo kwa pamoja inakuja asilimia 7. Halimashauri asilimia 0.3 Service Levy na zingine asilimia 15 kwa Wasimamizi wa mgodi na asilimia 15 kwa Kijiji, na Asilimia 70 kwa wachimbaji". Alieleza

DC Tano Mwera pia amebaini changamoto ya mikataba ya wachimbaji wadogo na Waajili wao ambao wanawaita wafadhili inaleta sinto fahamu ya mapato ya Serikali na  Waajili wao wanapochukua asilimia fulani kutokana na makubaliano yao baada ya viroba vya  mawe ya dhahabu kupatikana wao huona kama wanapunjwa, wakati Serikari haihusiki na mikataba yao binafsi na wafadhili wao.

DC Tano Mwera ametoa maelekezo kwa uongozi wa Mgodi, pamoja na uongozi wa Chama cha Wachimbaji wadogo Simiyu (SIMIREMA) kwenda mbali zaidi kwa kufatilia mikataba ya wachimbaji hao pamoja na wafadhili wao na pia gharama za uchimbaji kama gharama za Miti, kuchunguzwa kama haziwatendei haki wachimbaji wadogo waingilie kati.

Aidha, DC Tano Mwera  amesisitiza wanunuzi wote wa dhahabu lazima wawe na leseni ya ununuzi na lazima wauzie katika soko la Madini Mkoa wa Simiyu.

"Naagiza kamati ya Wilaya chini ya Mwenyekiti wake Afisa Madini Mkoa ndugu, Ayubu Samwel na Katibu wake Afisa Usalama wa Wilaya kufanya ufatiliaji wa karibu juu ya utoroshaji wa dhahabu kwenda nchi jirani ya Kenya na kukosesha Serikali mapato" alieleza DC.

Aidha, DC Tano Mwera hakufurahishwa na hatua za tahadhari dhidi ya Virus vya Corono zinazochukuliwa katika Mgodi huo huku akitishia kuufunga kutokana na kwenda tofauti na maelekezo yake aliyoyatoa awali ya kila anayeingia na anaye fanya kazi katika eneo la Mgodi lazima awe amevaa Barakoa, kitu ambacho hakikutekelezwa.

"Uvaaji wa Barakoa ni jambo la lazima. Nawataka wasimamizi wa Mgodi kuhakikisha kila mtu katika eneo la Mgodi anavaa Barakoa la sivyo nafunga Mgodi." Alieleza.

No comments:

Post a Comment

Pages