HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

May 10, 2020

MTANDAO WA WANAWAKE LAKIMOJA WATOA PONGEZI KWA WAMAMA WOTE

Na Mwandishi Wetu

MTANDAO wa Wanawake Laki Moja  (100,000  WOMEN) wenye lengo la kuunganisha na Wanawake, kupambana na Ukatili wa Kijinsia na Umasikini hapa nchini umetoa pongezi kwa akina Mama wote walio mstari wa mbele kwenye mapambano dhidi ya virusi vya Corona.

Pongezi hizo zimetolewa leo ambayo ni siku ya Kina Mama (Mother's Day )  ambapo wamekuwa mstari wa mbele katika mapambano.

"WanawakeLakiMoja tunawapongeza kina Mama wote wa Tanzania na duniani kwa ujumla. 
Kazi kubwa wanazozifanya za kubeba majukumu ya familia na jamii" ilisema taarifa yao.

Mtandao huo ambao unafanya kazi Tanzania nzima. Kwa sasa upo katika Mikoa 21.

Mtandao huo ulianza mapema mwezi Januari 2020 na makao makuu yake ni Jijini Mwanza.

Katibu wa Mtandao huo, Madam Josephine Ngoda alieleza kuwa, Wanawake wenye lengo la kujiunga na mtandao huo wanakaribishwa.

"Wanawake tunawakaribisha.  Unapaswa kujitambulisha pahala ulipo na unafanya nini na ujumbe kwa wanawake kisha kupakia ( ku post) katika mitandao yetu ya kijamii ikiwemo facebook na Instagram
 Facebook@wanawakelakimoja na Instagram@wanawakelakimoja"

No comments:

Post a Comment

Pages