Na Tiganya Vincent
HALMASHAURI
za Mkoa wa Tabora hadi sasa zimefanikiwa kutoa mikopo ya shilingi bilioni 1.3
kwa vikundi mbalimbali vya vijana , walemavu na wanawake.
Kauli
hiyo imetolewa jana na Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Msalika Makungu wakati wa
kikao cha Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Urambo.
Alisema
Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua ndio inaongoza kwa kutoa shilingi milioni 369
ikiwa ni sawa na asilimia 165 ya makusanyo yake ya ndani na Igunga ilitoa
mikopo ya shilingi milioni 180 ikiwa ni asilimia 150 ya mapato yake ya ndani.
Makungu
alisema Halmashauri ya Urambo ilitoa mikopo ya shilingi milioni 160 ikiwa ni
asilimia 139 , Manispaa ya Tabora ilitoa mikopo ya shilingi milioni 235 sawa na
asilimia 132 na Uyui ilitoa mikopo ya shilingi milioni 167 sawa na asilimia 109.
Alitaja
Halmashauri ya Wilaya ya Nzega ilitoa mikopo ya shilingi milioni 66.2 sawa na
asilimia 102 , Nzega Mji ilitoa mikopo ya shilingi milioni 90 sawa na asilimia
10 na Sikonge ilitoa mikopo ya shilingi milioni 125 sawa na asilimia 81.
Katibu
Tawala huyo wa Mkoa alizitaka Halmashauri kuhakikisha zinafuatilia vikundi
vyote vilivyopata mikopo kwa ajili ya kurejesha ili ziweze kusaidia vikundi
vingine katika shughuli za maendeleo.
Alisema
kwa upande wa Halmashauri ya Wilaya ya Urambo kuna jumla ya shilingi milioni
510.7 ambazo zilikopeshwa kwa vikundi vya wanawake , vijana na walemavu
hazijareshwa.
No comments:
Post a Comment