Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Denis Minja, akiwa amembeba mtoto aliyemuokoa kutoka ndani ya shimo la choo.
Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Kagera, Hamis Dawa.
Na Lydia Lugakila, Kagera
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Kagera limefanikiwa kumuokoa Mtoto mwenye umri wa mwaka mmoja aliyetelekezwa na kutupwa katika shimo la choo.
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Kagera limefanikiwa kumuokoa Mtoto mwenye umri wa mwaka mmoja aliyetelekezwa na kutupwa katika shimo la choo.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Kagera, Hamis Dawa, tukio hilo limetokea Mei 21 mwaka huu wilayani ngara mkoani Kagera ambapo jeshi hilo limefanikiwa kumwokoa mtoto huyo aliyekutwa ndani ya shimo la choo cha shule ya msingi Murugwanza.
Kamanda Dawa ametoa pongezi kwa askari wa jeshi hilo, Danis Minja, aliyemwokoa mtoto huku harakati za kumtunuku cheo kwa ajili ya ushujaa huo zikiendelea.
Amesema kuwa uchunguzi zaidi unaendelea ili kumbaini mhusika aliyefanya kitendo hicho cha kinyama.
Hata hivyo kamanda huyo ameitaka jamii mkoani Kagera kuacha mara moja vitendo vya utelekezaji wa watoto kwani vinaonekana kukithiri mkoani hapa.
No comments:
Post a Comment