Mwonekano wa
baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Alat Mkoa wa Pwani wakiwa katika chumba
amabcho kuna mitambo maalumu ambayo imetengenezwa kwa ajili ya kuchanganyia
madawa ya aina mbali mbali ikiwemo dawa kwa ajili ya kuulia mazalia ya
Mbu. (Picha na Victor Masangu).
Katibu wa Alat Mkoa wa Pwani, Musa Gama (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na waandishi wa habari mara baada ya
kumalizika kwa ziara ya kukagua miradi mbali mbali ya maendeleo katika halmashauri
ya Kibaha mji.(Picha na Victor Masangu).
VICTOR MASANGU, PWANI
KAMATI
ya jumuiya ya umoja wa serikali za mitaa ALAT Mkoa wa
Pwani imewaagiza watendaji na watumishi wa halmashauri kuhakikisha
wanaunga
mkono juhudi za serikali ya awamu ya tano kwa kuweka mipango madhubuti
ambayo itasaidia kusimamia miradi mbali mbali ya maendeleo ili
iweze kukamilika kwa muda uliopangwa bila ya kucheleweshwa kwa maslahi
ya
wananchi na Taifa kwa ujumla.
Hayo yalibainishwa na
Mwenyekiti wa Alat Mkoa wa Pwani Hatibu Chaulembo
wakati wa ziara ya kutembelea miradi mitatu ya kimikakati ikiwemo ujenzi wa
machinjio ya kisasa, ujenzi wa soko, pamoja na kiwanda cha kuzalisha dawa ya
kuulia mazalia ya mbu viuwadudu ilivyopo
katika halmashauri ya Mji Kibaha na kuongeza kuwa wameridhishwa na hatua ambayo
imefikia.
Aidha Mwenyekiti huyo alisema kwamba serikali ya awamu ya
tano imekuwa ikitenga fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbali mbali ya
maendeleo hivyo inatakiwa isimamiwe ipasavyo na kukamilika kwa wakati ili
kuweza kuwasaidia wanannchi wa maeneo mbali mbali katika Mkoa wa Pwani waweze
kupata fursa za ajira na wengine kujiajiri wao wenyewe.
“Sisi kama kamati ya Alat Mkoa wa Pwani tumefanya ziara ya
kukagua na kutembelea miradi mitatu ya kimikakati katika halmashauri ya mji
Kibaha ikiwemo Soko kubwa la kisasa, ijenzi wa machinjio ya kisasa pamoja na
kujionea shughuli mbalin mbali za uzalishaji amabzo zinafanyika katika kiwanda
cha viuadudu hivyo kwa pamoja tumerudhishwa na mwenendo mzima japo kuna mambo
mengine yanatkiwa yafanyiwe kaza zaidi,”alisema Chaurembo.
Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Wilaya
ya Kisarawe Musa Gama ambaye pia ni Katibu wa Alat Mkoa wa Pwani alimshukuru
Rais wa awamu ya tano Dk. John Pombe Magufuli kwa kutenga fedha kwa ajili ya
utekelezaji wa ujenzi wa miradi mbali mbali ambayo itaweza kusaidia kwa kiwango
kikubwa kuwasaidia wananchi kujikwamua kiuchumi na kuondokana na wimbi la
umasikini.
Gama alibainisha kuwa utekelezaji wa miradi mbali mbali ya
maendeleo ni njia moja wapo ya kuwaondolea wananchi wimbi la umasikini hivyo
juhudi ambazo zinafanywa na serikali ya awamu tano chini ya usimamizi mzuri
waRais Dk. John Pombe Magufuli hivyo kumamilika kwa miradi hiyo kutakuwa ni
chachu kubwa katika kukuza uchumi wa nchi.
“Mimi kama Katibu wa Alat Mkoa wa Pwani naweza kusema
nimejifunz amambo mbali mbali katika ziara hii amabyo tumeifanya katika
halmashauri ya mji wa Kibaha kwani nimeweza kujionea ujenzi wa machinjio
makubwa ya kisasa pamoja na soko jipya ambayo hivi vyote kwa pamoja vitaweza
kuleta mabadiliko chanya kwa wananchi pindi vitakapokuja kukamilika kw ahiyo ni
hatua kubwa sana ambayo imefanyika,”alisema Gama.
Nao baadhi ya wajumbe wa kamati YA Alat Mkoa wa Pwani
akiwemo Hamisi Dipakutile, Mshamu Munde pamoja na Jenipher Omolo alisema kwamba
serikali ya awamu ya tano imeweza kufanya mambo mengi katika sekta mbali mbali
hivyo wana imani kuwa katika siku za usoni miradi hiyo pindi ikikamilika
italeta maendeleo makubwa kwa wananchi.
No comments:
Post a Comment