HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

May 03, 2020

Rais Magufuli Ateua Bosi Mpya MSD

Rais John Magufuli.

Na Mwandishi Wetu

Rais John Magufuli amefanya uteuzi mwingine mpya kwa kumteua Brigedia Jenerali Dk. Gabriel Mhidize kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD).

Taarifa ya Ikulu iliyosainiwa leo na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu Chato, Gerson Msigwa ilisema, uteuzi wa Brigedia Jenerali Dk. Mhidize umeanza Mei 3, mwaka huu.

Taarifa hiyo ilisema kabla ya uteuzi huo, Brigedia  Jenerali Dk. Mhidize alikuwa Mkuu wa Hospitali ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ) Lugalo Jijini Dar es Salaam.

“Brigedia Jenerali Dk. Mhidize anachukua nafasi ya Laurean Bwanakunu ambaye uteuzi wake umetenguliwa.

Hata hivyo taarifa hiyo ya Ikulu haikueleza wazi sababu za kutenguliwa kwa Bwanakunu katika nafasi hiyo.

No comments:

Post a Comment

Pages