Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda. |
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, amewaelekeza watu wote
waliofunga Hotel, Migahawa na sehemu za biashara kutokana na hofu ya
Corona kuzifungua na kuanza kazi kama kawaida huku akiwataka waendelea
kuchukuwa tahadhari kwa kufuata maelekezo ya Wizara ya Afya.
RC
Makonda ametoa wito pia kwa Wale waliokimbilia mikoani kwa kuhofia
Corona kuhakikisha wanarudi na kuendelea na majukumu yao kama kawaida.
Aidha
RC Makonda ametangaza siku ya Jumapili ya wiki hii kuwa siku ya Sherehe
na Shukrani kwa Mungu kwa kutukinga na Janga la Corona ambapo ameeleza
kuwa atafurahi kuona kila mmoja anasherekea siku hiyo.
"Rais
Magufuli ametupa siku tatu za kumshukuru Mungu wetu, naamini kila mmoja
atafanya ibada ya Shukrani lakini mimi nimeomba Jumapili kila Mtu apige
shangwe na vigelegele ikiwa ni ishara ya Shukrani kwa Mungu wetu kwa
Makuu aliyotutendea, Mtakumbuka historia ya Wana wa Israel walichofanya
kwenye ukuta wa Yerico, kwaiyo kama wewe una mziki wako nyumbani piga
kelele uwezavyo na Tarehe 25 tunaendelea kuchapa kazi kama kawaida"
Alisema RC Makonda
No comments:
Post a Comment