NA IRENE MARK
MKURUGENZI Mtendaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF), Ladislaus Mwamanga, amesema kiasi cha Sh. Trilioni 2.032 zitagaiwa kwa walengwa kuanzia Juni mwaka huu, kwa njia za kielektroniki.
Alisema fedha hizo zitatumika kugawa ruzuku kwa kaya maskini zaidi zilizokidhi vigezo na nyingine zitatekekeza miradi ya maendeleo kwenye sekta za afya, elimu na maji kwa ngazi ya kitongoji.
Alisema katika kukabiliana na changamoto walizokumbana nazo kwenye utekelezaji wa kipindi cha kwanza cha TASAF awamu ya tatu, hivi sasa malipo yote yatafanyika kielektroniki ili kuongeza ubora wa huduma na kuwafikia walengwa halisi kwa njia ya simu zao za mkononi au akaunti ya benki.
Mwamanga aliyezungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Dar es Salaam jana, alisema kipindi cha pili, kaya milioni 1.4 zilizokidhi vigezo vya umaskini kutoka vijiji vyote Tanzania vitafikiwa.
"Hatuwapi ruzuku tukawaacha, hapana tunashirikisha kwenye kubuni miradi ya kuboresha miundombinu kwenye sekta za afya, elimu na maji.
"...Kabla ya kuamua kufanya malipo kielektroniki tulifanya utafiti kwenye wilaya 16 na kufanya malipo kwa njia ya mtandao. Mafanikio yalionekana na sasa utaratibu huu utatumika nchi nzima kila kijiji na mlengwa atalazimika kuwa na simu au namba ya akaunti," alisema mkurugenzi huyo.
Alizitaja halmashauri hizo kuwa ni Mpanda, Ilala, Kinondoni, Arusha, Temeke, Kigoma Manispaa, Bagamoyo, Songea Manispaa, Kisarawe, Kilwa, Muheza, Mkuranga, Bahi, Urambo, Siha na Unguja.
"Hadi Januari mwaka huu, walengwa 55,539 kati ya 102,299 sawa na asilimia 59 kwenye halmashauri hizo walianza kupokea ruzuku kwa njia ya mtandao ambazo ni simu na akaunti za benki," alisema Mwamanga.
Alisema licha ya changamoto chache anazokumbana nazo mlengwa, kwa miaka miwili ya majaribio, mfumo wa malipo kielektroniki umeonesha ufanisi kwa kupunguza gharama za uendeshaji.
Hata hivyo Mwamanga aliwataka walengwa hao kuhakikisha wanapata namba ya utambulisho wa NIDA na kusajili laini zao za simu na kufungua akaunti benki ili kuepusha usumbufu a upotevu wa fedha zao.

No comments:
Post a Comment