Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, (watatu kushoto) akikagua hatua za utekelezaji wa mradi wa kufua umeme wa Julius Nyerere (JNHPP) utakaozalisha Megawati 2,115, unaojengwa na kampuni ya Yapi Merkezi, May 14, 2020. ( Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Na Mwandshi Wetu
Na Mwandshi Wetu
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekagua
maendeleo ya ujenzi wa mradi wa kufua umeme wa Julius Nyerere (JNHPP) utakaozalisha
Megawati 2,115 na amemwagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania
(TANESCO) Dkt. Tito Mwinuka asimamie mradi huo ili ukamilike kwa wakati.
Vilevile, Waziri Mkuu amemwagiza mkandarasi anayejenga
mradi huo aukamilishe kwa wakati kwa sababu imebainika kuwa mvua zinazoendelea
kunyesha nchini haziathiri utekelezaji wa ujenzi huo.
Waziri Mkuu ametoa
maagizo hayo leo (Alhamisi Mei 14, 2020) akiwa katika ziara ya kukagua hatua za
utekelezaji wa mradi huo. Amesema ameridhishwa maedeleo ya ujenzi wa mradi huo
mkubwa wa kimkakati.
“Nimetembelea eneo la
mradi na kujionea shughuli zote zinazoendelea, kazi inayofanyika ni ya uhakika
huku kukiwa na matumaini makubwa ya kukamilisha mradi mapema kabla ya muda
uliopangwa.”
Mradi wa umeme wa
maporomoko ya maji ya Mto Rufiji unajengwa na kampuni ya Arab Construction kwa
pamoja na kampuni ya Elsewedy Electric zote za kutoka nchini Misri. Mradi huo
unatarajiwa kuzalisha Megawati 2,115 ambazo zitaingizwa kwenye grid ya Taifa na
kuifanya nchi kuwa na umeme mwingi na wa uhakika.
Mbali na kuliwezesha
Taifa kuwa na umeme wa uhakika, pia mradi huo umewezesha kupungua kwa
changamoto ya ajira baada ya Watanzania wengi wakiwemo wakandarasi kupata ajira
za kudumu na za muda mfupi.
Kukamilika kwa utekelezaji wa mradi huo, kutaiwezesha
Tanzania kuzalisha kiasi kikubwa cha umeme kitakachosaidia kutekeleza miradi
mikubwa ya kimkakati ikiwemo ujenzi wa uchumi wa viwanda na mradi wa reli ya
kisasa.
Hafla ya utiaji saini ya Mkataba wa Ujenzi wa Mradi
ilifanyika jijini Dar es Salaam, tarehe 12 Desemba, 2018 na kushuhudiwa na Rais
Dkt. John Pombe Magufuli na Waziri Mkuu wa Misri Dkt. Mostafa Madbouly. Mradi
huu ni njia sahihi ya kufikia Uchumi wa Viwanda ifikapo mwaka 2025.
No comments:
Post a Comment