HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

May 30, 2020

WENYE VIPAJI VYA UCHORAJI WAJITOKEZE


 Na Denis Mlowe, Iringa

VIJANA wenye vipaji vya kuchora mkoani Iringa wametakiwa kujitokeza kwa wingi kwenye mradi mpya wa uchoraji uliopewa jina la The Streets of Iringa Krafts wenye nia kuibua na kuendeleza vipaji vya uchoraji na kuzalisha ajira zaidi.

Wito huo umetolewa na mdau wa maendeleo, Ahmed Salim Abri (pichani) kwa lengo la kuwawezesha vijana kutumia kipaji cha uchoraji katika kukuza ajira mkoani hapa ikiwa ni sehemu ya moja ya mikakati ya kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya tano ya vijana kufanya kazi.

Ahmed Abri  ambaye pia ni mkurugenzi wa mgahawa wa kisasa wa The Koffee Shop ulioko mjini Iringa alisema kuwa mtaani kuna vijana wengi wenye vipaji vya kuchora hivyo ni wakati wao sasa kuweza kujitokeza kwa wingi kuonyesha kwenye jamii vipaji hivyo katika uchoraji mambo yanayohusu mkoa wa Iringa.

Alisema kuwa kuna vijana  wenye uwezo maalum huwa wana vipaji katika taaluma mbali mbali hivyo kuna haja ya kuwapa usaidizi kuvikuza na kwa kuanza wenye vipaji vya uchoraji wanatakiwa kujitokeza kwani ni moja ya fani ambayo imesaulika sana mkoani hapa ukilinganisha na fani nyingine zikiwemo mpira wa miguu.

“Mimi kama mimi nimeona kuwa kuna vipaji sana vya uchoraji mkoani hapa hivyo ndio wakati sahihi wa kuvikumbuka kwani kuna watu wenye uwezo maalum mara kwa mara wamekuwa wakikosa watu wa kuwaunga mkono hasa katika jamii hivyo wajitokeze kwa wingi kuonyesha uwezo wao” alisema


Kwa sasa ameitaja jamii kuwapa kipaumbele ili kuhakikisha vipawa vyao vinakuzwa kama watu wengine katika jamii.

Aidha Ahmed ametoa wito kwa jamii kujitokeza na kuwatambua pamoja na kusaidia ku
endeleza vipaji vya watu wanaoishi na uwezo maalum ili kuboresha vipaji vyao ambavyo vimekuwa vikipotea katika mazingira ambayo yanasababishwa na kukosa msaada kutoka kwa jamii na kuacha wakishindwa kutumia vipawa vyao.


Aliongeza kuwa watu wa dini huamini kipaji mtu hupewa na MUNGU katika uumbaji ni sehemu ya uwezo wa kufanya jambo fulani kwa ngazi ya juu na kipaji kinaweza kuwa cha kimwili au cha kiakili na uwezo wa kuzaliwa nao wa kufanya kazi fulani lakini kinaweza kikaendelezwa au kutoendelezwa na kipaji hakirithishwi wala huwezi kujifunza sehemu yoyote.

Abri alisema kuwa uchoraji ni uwezo, ujuzi ulioendelezwa, maarifa au uhodari na mtazamo alionao mtu ambao uko na asili ya ndani ya kipaji ni kuonyesha ujuzi na mafanikio, ambayo huwakilisha maarifa au uwezo unaopatikana kupitia kujifunza.

“Kipaji huweza kuishi ndani ya mtu bila kupotea kadiri kinavyozidi kutumiwa ndivyo huzidi kuimarika mfano wa vipaji ni kuchora, kutambua na kuvumbua vitu kwa haraka hivyo wafatilie ukurasa wa  ‘ The Streets Of Iringa Krafts’ kwenye mtandao wa Instagram ambapo maelezo zaidi yatatolewa’ Alisema

Alisema kuwa vijana hao watatumika katika kutangaza utalii wa mkoa wa Iringa hasa katika tasnia ya uchoraji hivyo lengo ni kuwasaidia kupata ajira na kutopoteza vipajia vyao ambavyo wamepewa na mola viweze kuwasaidia kupata ajira.

No comments:

Post a Comment

Pages