HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 04, 2020

AFRICAB yatoa msaada wa matanki 100 Serikalini kukabiliana na Corona

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akiangalia matanki ya kunawia mikono yaliyotolewa na kiwanda cha utengenezaji vifaa vya umeme cha AFRICAB, kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa kiwanda hicho Mansoor Moiz.
 Wadau wa shule na vyuo wakipakia matenki kwa ajili ya kuyapeleka mahali husika.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Ndalichako, akizungumza wakati wa hafla ya kupokea matanki ya kunawia mikono yaliyotolewa na kiwanda cha kutengeneza vifaa vya umeme cha AFRICAB.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Ndalichako, akikata utepe wakati wa hafla ya kupokea matanki ya kunawia mikono yaliyotolewa na kiwanda cha kutengeneza vifaa vya umeme cha AFRICAB kwa ajili ya kuwawezesha wanafunzi na wanavyuo jijini Dar es Salaam kunawa mikono ili kukabiliana na janga la homa mapafu inayosababishwa na virusi vya Corona.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako, akiwa katika picha ya pamoja na familia ya inayomiliki kiwanda hicho, kulia  kwa waziri ndalichako ni mkurugenzi wa AFRICAB Mansoor Moiz, kushoto kwake na mkuu wa wilaya ya temeke Felix Lyaniva pamoja na Afisa elimu mkoa.


Na Mpiga Picha Wetu 
 

SERIKALI kupitia Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia imepokea msaada wa matanki 100 kutoka kampuni ya utengenezaji wa vifaa vy umeme ya AFRICAB maalumu kwa ajili ya kuwawezesha wanafunzi na wanavyuo jijini Dar es Salaam kunawa mikono ili kukabiliana na janga la homa mapafu inayosababishwa na virusi vya Corona.

 Akipokea na kisha kukabidhi matanki hayo yenye jamani ya Sh Milioni 50, Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof.Joyce Ndalichako mbali na kushukuru kwa msaada huo, alisema msaada huo umekuja wakati muafaka ambapo vyuo na baadhi ya shule nchini  zimefunguliwa na kwamba itawawezesha wanafunzi kujikinga dhidi ya ugonjwa huo wa Covid-19.

Alisema msaada wa matanki hayo yenye ujao wa Lita 1000 kila moja yalitotolewa kwa shule 10 za Sekondari za Serikali na 57 kwa shule za sekondari za binafsi na vyuo 13 ni muhimu kwa Serikali hasa wakati huu ambapo vita dhidi ya ugonjwa huo unaendelea.

"Niwapongeze AFRICAB msaada huu muhimu kwa ajili ya kinda afya za wanafunzi wetu, niwaombe wadau wengine muige mfano huu kwa ajili ya manufaa ya watu wote wa taifa hili" alisema Prof.Ndalichako.

Aidha alisema licha ya hatua mbalimbali zinazoendelea kuchukuliwa na Serikali katika napambana dhidi ya Corona, wananchi nao wanapaswa kuchukua tahadhari hizo huku wakiendelea kuchapa kazi.

Kwa upande wake Meneja Masoko wa AFRICAB David Tarimo, alisema msaada umetolewa kwa lengo la kuunga mkono kurudi za Serikali katika kukabiliana na Corona na kusisitiza kuwa wao kama wadau wa maendeleo na wawekezaji wazalendo huo ni wajibu wao wa kimsingi.

Alisema mapambano dhidi ya Corona ni wajibu wa kila mmoja na kwamba wao kama AFRICAB wanatambua nini kinafanywa na Serikali katika kukabiliana na ugonjwa huo unaoisumbua dunia kwa sasa.

Aidha alisema mbali na msaada huo, AFRICAB itaendelea kushirikiana na Serikali katika masala mbalimbali ya kimaendeleo huku ikitarajia kujenga cha uzalishaji wa dawa za binadamu hivi karibuni.

Awali Mkurugenzi Mwenza wa kiwanda hicho Mohammed Ezz alisema amemshukuru Rais John Magufuli kwa kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji yanayokiwezesha kiwanda hicho kutekeleza majukumu yake ipasavyo.

No comments:

Post a Comment

Pages