Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Joachim Wangabo.
Na Mwandishi Wetu
Mkuu wa mkoa wa Rukwa
Mh.Joachim Wangabo amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi kuwawajibisha
watumishi wote walioisababishia halmashauri hiyo kupata hati yenye shaka na
kumpatia taarifa ya hatua alizochukua kwa watumishi hao ndani ya siku saba kabla
ya mabaraza ya madiwani kuvunjwa.
Amesema kuwa kwa
mujibu wa maelekezo ya Katibu Mkuu Ofisi ya Raisi Tawala za Miko ana Serikali
za Mitaa (OR-TAMISEMI) yaliyotolewa tarehe 24, April, 2020 kuhusu kushughulikia
hoja na mapendekezo ya CAG, pamoja na mambo mengine imeelekezwa kuwa Halmashauri
zilizopata Hati yenye Shaka zimepoteza sifa za kupatiwa fedha za utekelezaji wa
miradi ya kimkakati katika kipindi cha miaka mitatu ijayo na hivyo kuchelewesha
maendeleo kwa wananchi.
“Kwa kupata hati
yenye shaka, halmashauri ya wilaya ya Nkasi inapoteza sifa za kupatiwa fedha za
utekelezaji wa miradi ya kimkakati ambayo lengo lake ni kupoteza mapato katika
halmashauri, hii ni adhabu kubwa sana katika halmashauri yetu, haipendezi,
pengine wengine walikuwa wanaichukulia kijuu juu, miradi ya kimkakati ni miradi
mukubwa ambayo halmashauri zimepewa nafasi ya kubuni na kupatiwa fedha ya
kutekeleza, kama ni stendi za mabasi, maghala au kumbi zamikutano,” Alisema.
Na kuongeza kuwa ,”
Hawa waliotufikisha hapa, hawawezi kuachwa hivi hivi, ni lazima wachukuliwe
hatua kali za kinidhamu na Mkurugenzi nimekupa siku saba, uwe umetoa adhabu
hii, nipate taarifa ndani ya siku saba, iwe nimepata taarifa ya namna hawa watu
watakavyoshughulikiwa kinidhamu, hatuwezi kuendelea namna hii watu wanafanya
mzaha, wanafanya uzembe, halafu halmashauri inabeba mzigo wa hawa watu wachache
wazembe kwanini?” Alikemea.
Wakati akieleza miongoni
mwa sababu zilizosababisha halmashauri hiyo kupata Hati ya Mashaka kwenye
hesabu za kuishia tarehe 30, Juni 2019 Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo alisema
kuwa Ukaguzi wa mtiririko wa fedha (Cash Flows Statements) kwenye kitabu cha
hesabu ulionesha kuwa na upungufu wa shilingi 2,528,347,000/=.
“Ukaguzi wa Mtiririko
wa fedha kwenye kitabu cha hesabu ilibainika kuwa Halmashauri imeonesha
mtiririko wa fedha uliotoka kuwa Shilingi 16,827,818,000 ikiwa ni mishahara,
malipo ya vibarua na haki mbalimbali za watumishi, hata hivyo kwenye mchanganuo
ilionekana madai ya watumishi yamepungua kwa Shilingi 383,690,000 hivyo kufanya
madai ya watumishi kuoneshwa pungufu kwa jumla ya Shilingi 2,528,347,000/=,”
Alifafanua.
Aliongeza kuwa kwa upande
wa magari na pikipiki, mali za halmashauri, halmashauri ilionesha jumla ya
Shilingi 554,292,000/= lakini baada ya daftari la mali za kudumu kupitiwa
ilionesha jumla ya shilingi 612,940,420 na khivyo kuonesha upungufu wa Shilingi
58,648,420/=.
Kwa upande wake Afisa
Serikali za Mitaa mkoa wa Rukwa Albinus Mgonya alisema kuwa kati ya Halmashauri
185 zilizokaguliwa kwa hesabu zilizoishia 30 Juni 2019, Halmashauri 176
zilipata Hati Inayoridhisha na Halmashauri 9 zilipata Hati yenye Shaka ikiwemo
Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi huku hoja zilizoibuliwa kwa kipindi cha mwaka wa
fedha 2018/2019 ni hoja 32 na hoja za nyuma zilizokuwa bado hazijafungwa ni 52.
No comments:
Post a Comment