Wachezaji wa timu Rajaa FC wakiwa katika mazoezi kwa ajili ya kujiandaa na mashindano mbalimbali.
Na Denis Mlowe
TIMU
ya soka ya Rajaa Fc yenye maskani yake Kariakoo jijini Dar es Salaam
inayoshiriki ligi mbalimbali za soka zinazondaliwa jijini Dar es Salaam
imejipanga kufanya vyema katika mashindano yoyote ikiwemo ligi ya
kutafuta bingwa wa mkoa wa Dar es salaama katika kuelekea madaraja ya
juu zaidi nchini.
Wakizungumza
na mwanahabari hizi,Kocha Mkuu wa timu hiyo, Kassim Ramadhani na
viongozi wake Mohamed Abri walisema kuwa mara baada ya serikali
kutangaza baadhi ya michezo kuendelea kama kawaida timu hiyo iko katika
mazoezi makali yanayofanyika katika viwanja vya JK na Uhuru taifa
kujiwinda na mashindano yoyote yatakayojitokeza jijini Dar es Salaam.
Kocha
Ramadhani alisema kuwa wamejipanga katika suala zima la mazoezi kwani
changamoto ilikuwa ni gonjwa la Covid 19 ila kwa sasa tumeanza mazoezi
makali kwani wachezaji wengi walikuwa tu majumbani huku baadhi wakifanya
mazoezi binafsi tofauti na timu hivvo kwa sasa ni mazoezi mwanzo
mwisho.
Alisema
kuwa timu hiyo imekuwa timu mojawapo ndogo zenye uongozi uliojipanga
vyema kuhakikisha inafanya vizuri kwenye ligi mbalimbali zinazoandaliwa
jijini hapa kwa lengo la kujiweka vyema na kuanza maandalizi ya kutafuta
bingwa wa mikoa inayotarajiwa kuanza wakati wowote.
Alisema
kuwa wachezaji wa timu hiyo wamekuwa katika hali nzuri na ni vijana
wenye nia ya kufanya vyema zaidi katika soka la Tanzania nje hivyo kuwa
na njaa ya mafanikio chini ya uongozi bora kabisa wa Mkurugenzi wa timu
Mohamed Abri na nahodha wake Salim Salehe Abri.
Aliongeza
kuwa timu hiyo imekuwa ikishiriki mechi mbalimbali za ndani ya jiji na
nje ya jiji ambapo walicheza mechi na timu ya Ligi Kuu ya Lipuli Fc
mkoani Iringa na kuleta upinzani mkubwa hali ambayo iliwapa nguvu ya
kuweza kufanya vyema katika mashindano yoyote watakayoshiriki.
Kwa
upande wake, Nahodha wa timu hiyo, Salim Salehe Abri alisema kuwa Klabu
hiyo yenye wachezaji vijana na wenye hali wako tayari kwa mashindano
yoyote watakayoshirki kwani wachezaji wako katika hali nzuri na kuwa na
kila kitu ambacho wanahitaji kwa sasa ikiwemo vifaa na jezi za uhakika
kushiriki mashindano mbalimbali.
Abri
aliwataka wachezaji wa timu hiyo kufanya mazoezi kwa moyo kwa lengo la
kuiletea mafanikio timu biyo na kufanikisha malengo waliyojiwekea ya
kuchukua ubingwa kwa kila mashindano watakayoshiriki jijini Dar es
Salaam.
Alisema
kuwa kwa sasa timu hiyo kwa kushirikiana na uongozi na wachezaji
wameweka mikakati ya kufanya vyema nchini kwa ujumla hali ambayo
inatokana na ushirikiano mzuri na viongozi wa timu na wachezaji pamoja
na mashabiki wanaowaunga mkono popote wanapokwenda
Abri
ambaye ameshiriki ligi mbalimbali za soka nchini amekuwa mstari wa
mbele katika kuwapa moyo wachezaji chipukizi wa timu hiyo kuweza
kuonyesha zaidi vipaji kwa lengo kujiuza zaidi katika ligi mbalimbali
duniani kwa kupitia timu ya Rajaa yenye mlengo wa kukuza vipaji za vya
soka zaidi.
No comments:
Post a Comment