HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 10, 2020

Benki ya CRDB yawaalika wanahisa katika Mkutano Mkuu wa kihistoria wa Mwaka 2020

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (wa pili kushoto) akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano wa kuwakaribisha wanahisa wa Benki ya CRDB katika Mkutano Mkuu wa 25 utakaofanyika kupitia mtandao (virtual meeting) tarehe 27 Juni 2020. Kutoka kulia ni Katibu wa Benki, John Rugambo, Afisa Mkuu wa Fedha, Fredrick Nshekanabo, na Mkurugenzi wa Mawasiliano, Tully Mwambapa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela, akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano wa kuwakaribisha wanahisa wa Benki ya CRDB katika Mkutano Mkuu wa 25 utakaofanyika kupitia mtandao (virtual meeting) tarehe 27 Juni 2020. Pamoja pichani ni Afisa Mkuu wa Fedha, Fredrick Nshekanabo.


Na Mwandishi Wetu

BENKI ya CRDB inatarajia kufanya Mkutano Mkuu wa Wanahisa wake kwa njia ya mtandao Juni 27,2020.

Awali mkutano huo ulipamgwa kufanyika Mei 16 mwaka huu lakini uliahirishwa kutokana na maradhi ya homa kali ya mafua yanayosababishwa na Virusi vya Corona (COVID19). kuingia nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari kwa njia ya mtandao jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB, Abdulmajid Nsekela alisema lazima wanahisa wote washiriki mkutano huo kwa kuw ni haki yao.

"Tunafahamu kuwa huu ni utaratibu mpya kwa hivyo kipaumbele cha kwanza ni kuhakikisha kuwa wanahisa wanapata haki yao ya kushiriki kikamilifu kwenye Mkutano Mkuu kwa kuchangia mada mbalimbali, kupiga kura, kuuliza maswali na kuwasilisha michango mingine," alisema Nsekela.

Alibainisha kwamba agenda mbalimbali zitajadiliwa katika mkutano huo ikiwamo uwasilishaji wa ripoti za mwaka na taarifa za fedha, kupitisha pendekezo la gawio, malipo ya bodi, uteuzi wa wajumbe huru wa bodi na uteuzi wa wakaguzi wa nje.

Kwa mujibu wa Nsekela, mkutano huo pia utatoa fursa kwa wanahisa wengi zaidi kushiriki popote waliopo huo.

"Natoa shime kwa wanahisa wote wa Benki ya CRDB kutumia mfumo wa fomu za uwakilishi “Proxy Forms” kwa kupakua fomu hiyo kwenye mtandao wetu wa www.crdbbank.co.tz ili kupiga kura kabla ya mkutano," alisema Nsekela.

No comments:

Post a Comment

Pages