Mkuu wa Wilaya ya Momba - Juma Said
Irando (wapili kushoto) akitoa neno la shukrani baada ya kukabidhiwa
vifaa vya ujenzi ikiwemo nondo, mbao za kenchi na mifuko 171 ya saruji.
Wakwanza kushoto ni Kaimu Meneja
wa NMB Kanda ya Nyanda za Juu - Hamadan Silliah.
Na Mwandishi Wetu
Benki ya NMB imekabidhi vifaa vyenye thamani ya Shilingi Milioni 5 kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Afya
cha Makambini Halmashauri ya Mji wa Tunduma wilayani Momba mkoani Songwe kusaidia kukabiliana
na janga la ugonjwa hatari wa COVID-19.
cha Makambini Halmashauri ya Mji wa Tunduma wilayani Momba mkoani Songwe kusaidia kukabiliana
na janga la ugonjwa hatari wa COVID-19.
Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo kwa niaba ya Meneja wa NMB Kanda ya Nyanda za Juu,
Meneja wa NMB Tawi la Mbalizi Road - Hamadan Silliah amesema msaada wa vifaa hivyo ni moja kati ya
mpango wa NMB ya kutenga sehemu ya faida yake katika kusaidia huduma za kijamii.
Silliah amesema kuwa Benki ya NMB Kanda ya Nyanda za Juu ilipokea maombi ya kusaidia ujenzi wa
kituo hicho na kwamba moja kati ya sera za NMB kurejesha faida katika huduma za kijamii ni pamoja na
kusaidia katika kukabiliana na majanga na huduma za Afya.
Amesema kutanuka kwa huduma za Benki hiyo kumeongeza pia uwepo wa huduma za NMB mkononi
kupitia simu za kiganjani na hii imesaidia kufanya muamala kwa njia za Kidijitali ikiwa ni moja ya sehemu
ya kujikinga na ugonjwa wa CORONA.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya mji wa Tunduma Bi. Regina Bieda amesema
ujenzi wa kituo hicho kinachotarajiwa kuwa na wodi mbili za akina mama na wanaume kinatarajia
kugharimu kiasi cha Sh.Milioni 95 hadi kukamilika kwake.
Akizungumza mara baada ya makabidhiano hayo Mkuu wa Wilaya ya Momba Juma Said Irando
amesema kuwa Benki ya NMB imekuwa na mchango mkubwa katika huduma za kijamii na kuwa msaada
katika kituo hicho cha Afya ni Mahsusi kwa magonjwa ya milipuko.
Amesema kituo hicho kipo mpakani ambayo ni njia kuu kuelekea nchi za SADC hivyo kumekuwa na
muingiliano wa wageni kutoka nchi zilizopo kusini na DRC Kongo na kuwa awali kituo hicho kilitengwa
kwa ajili ya EBOLA na sasa kinaboreshwa kutokana na ugonjwa hatari wa COVID-19.
No comments:
Post a Comment