Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Juma Aweso, akipiga makofi mara baada ya kumtwika ndoo ya maji kichwani
Mbunge wa Kibaha Vijijini, Hamoud Jumaa, baada ya kukamilika kwa
mradi wa maji katika kijiji cha Kipangege kilichopo kata ya Soga Wilayani
Kibaha ambao tayari umeshaanza kutoa huduma ya maji safi na salama (Picha Victor Masangu).
Mbunge wa Kibaha vijijini Hamoud Juma kushoto akitoa maelezo
mafupi kwa Naibu Waziri wa Maji na Umwagiiaji kuhusiana na mwenendo mzima wa
mradi huo wa maji katika kijiji cha Kipangege kilichopo kata ya Soga.
Victor Masangu, KIBAHA
WANANCHI wapatao 319 kutoka kijiji cha Kipangege kilichopo kata ya Soga
Wilaya ya Kibaha Mkoa wa Pwani ambao walikuwa
wanasumbuka usiku na mchana kwa ajili ya kutafuta maji safi na salama
hatimaye wameondokana na changamoto hiyo baada ya kukamilika kwa mradi wa maji ambao umegharimu
kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 150.
Hayo yamebainishwa na Naibu Waziri wa maji na umwagiliaji Juma Aweso wakati
wa ziara yak eta kikazi katika Wilaya ya Kibaha
Mkoa wa Pwani kwa ajili ya kukagua miradi mbali mbali ya maji na kutoa
muda wa siku saba kwa uongozi wa Wakala wa
usambazaji wa maji na usafi wa mazingira vijijini Mkoa wa Pwani (RUWASA)
kuhakikisha wanatekeleza maagizo yake aliyoyatoa ikiwemo na ufungaji wa tanki kubwa la maji na
kukemea vitendo vya ubadhilifu katika mradi huo.
“Nilikuja hapa mara ya kwanza kwa ajili ya kujionea mradi huu na niliambiwa
kuwa ulikuwa na chanagamoto mbali mbali lakini
kwa leo hii imeamua kuja kuangalia utekelezaji wa maagizo ambayo
niliyatoa juu ya upatikanaji wa maji kwa wananchi hawa, lakini sambamba na hilo nimejionea maji
yakitoka ili naagiza kwa mamlaza zinazohusika kufunga tanki la maji ili
kuondokana na changamoto ya maji kutoka
kwa mgao,”Alisema Aweso.
Aweso alibainisha kwamba lengo kubwa la serikali ya awamu ya tono ni kuhakikisha
kwamba inasimamia na kutekeleza kwa wakati
miradi mbali mbali ya maji ili kuweza kuwaondolea kero wananchi ambao
wakati mwingine wamekuwa wakisumbuka kwa kutembea umbari mrefu kwenda katika maeneo mengine
kutafuta huduma ya maji.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa kijiji cha Kipangege alisema
kwamba licha ya mradi
kukamilika lakini bado kuna kero
kubwa kwa wananchi kupata maji kwa mgao hivyo wameziomba mamlaka
zinazohusika kulivalia njuga suala, huku Mbunge wa Jimbo la Kibaha Vijijini Hamoud Jumaa akipongeza
juhudi zilizofanywa na watendaji wa Dawasa na Ruwasa katika suala la
upatikanaji wa maji safi na salama kwa
wananchi.
Naye Kaimu Meneja wa RUWASA Mkoa wa Pwani Injinia Beatrice Kasimbazi amekiri na kusema kwamba
mradi ho ulianza utekelezaji kwa
kipindi kirefu tangu mwaka 2014 ambapo
umeweza kukamilika mwaka huu kutokana na ushirikiano ambao wameufanya
baina yao pamoja na Dawasa kwa
kuzirekebisha kasoro zilizokuwepo ikiwemo changamoto ya pampu pamoja na chanzo
za maji.
"Huu mradi wa kikiji cha Kipangege kama nilivyoeleza hapo awaliulianza
kufanyika tangu mnamo mwaka 2014 lakini kutokana na kuwepo kwa changamoto mbali mbali kutoka kwa
mkandarasi ambaye alipewa dhamani ya kuutekeleza alikuwa anamapungufu
ndipo tukaamua kushirikiana bega kwa
bega na wenzetu wa Dawasa katika kukabiliana na kasoro ambazo zilikuwa
zimejitokeza katika kipindi cha nyuma na
hatimaye kuweza kuzitafutia ufumbuzi,"alsiema Baatrice.
KUKAMILIKA
kwa mradi wa maji katika kijiji cha Kipangege Wilayani
Kibaha ni moja ya hatua kubwa ya kuunga
mkono juhudi za Rais wa awamu ya tano Dr
John Pombe Magufuli ambayo itakuwa ni mkombozi katika kumtua mama ndoo
kichwani sambamba na kuwaondolewa wananchi hao adha kubwa ya kutafuta
maji usiku na mchana.
No comments:
Post a Comment