Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa NMB – Filbert Mponzi (Pili
kulia) akimkabidhi mfano wa hundi ya shilingi Bilioni Tatu Mkuu wa
Wilaya ya Handeni – Godwin Gondwe maalumu kwaajili ya vikundi vya
wakulima na wasindikaji wa zao la Muhogo Wilayani
Handeni Mkoani Tanga. Wengine kwenye picha ni Mkurugenzi wa Benki ya
Maendeleo ya Kilimo (TADB) – Japhet Justin (Pili kushoto), Mwenyekiti wa
Wakulima wa zao la Mihogo nchini Tanzania, Mwantum Mahiza, Mkurugenzi
Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni,
William Makufwe na Meneja wa NMB Kanda ya Kaskazini, Aikansia Muro
(Kulia).
Na Mwandishi Wetu
Katika juhudi za kuinua Sekta ya Kilimo nchini, Benki ya NMB kwa kushirikiana na Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB) wametoa shilingi Bilioni 3 kwa wakulima wadogo wa zao la muhogo Wilayani Handeni, ili kuwawezesha wakulima kukopesheka kirahisi.
Akizungumza katika mkutano na wakulima hao eneo la Mkata Wilaya ya Handeni, Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa NMB, Filbert Mponzi alisema mkopo huo wenye riba nafuu utawanufaishawakulima 421 ambao watakuwa katika makundi 43. “Shilingi bilioni 3 ni fedha nyingi, hivyo mzitumie vizuri ili na wengine waweze kufaidika.
Huu niuhamasishaji wa uwekezaji katika zao la muhogo ili kuwawezesha wakulima kujiongezea kipato na wakati huo kuendana na soko la China,” alisema Mponzi.
Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Godwin Gondwe aliishukuru Benki ya NMB kwa mkopo huo huku akisema katika kutatua changamoto ya masoko ya zao hilo, kiwanda cha kusindika kinatarajiwa kuanza kazi miezi michache ijayo na taratibu zinaendelea ili kuweza kulipata soko la china.
Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Godwin Gondwe aliishukuru Benki ya NMB kwa mkopo huo huku akisema katika kutatua changamoto ya masoko ya zao hilo, kiwanda cha kusindika kinatarajiwa kuanza kazi miezi michache ijayo na taratibu zinaendelea ili kuweza kulipata soko la china.
Akielezea harakati za Wilaya katika kuhamasisha zao la muhogo, Mwenyekiti wa Umoja wa Wazalishaji na Wasindikaji wa Muhogo Tanzania (TACAPPA), Bi Mwantumu Mahiza alisema zao la muhogo katika wilaya ya Handeni limekuwa la kibiashara kutokana na usafirishwaji wa muhogo mbichi kwa wingi kwenda Dar es Salaam.
Kwa miaka kadhaa, kilimo kimekuwa na mchango mkubwa katika uchumi wa Tanzania hasa katika upatikanaji wa chakula, biashara ya mazao nje ya nchi, kusaidia upatiakaji wa malighafi za viwanda vya ndani na kutoa ajira kwa Watanzania.
No comments:
Post a Comment