Diwani wa Kibamba aliyemaliza muda wake kupitia Chadema, Ernest Mgawe (kushoto), akimkabidhi mmoja wa viongozi wa chama hicho ripoti maalumu ya utekelezaji wa majukumu mbalimbali ambayo aliyafanya wakati wa uongozi wake. (Picha na Victor Masangu).
Diwani wa Kibamba ambaye amemaliza muda
wake kupitia tiketi ya chama cha demokrasia na maendeleo (C akizungumza na
viongozi wa chama hicho pamoja na wanachama wakati wa halfa fupi ya (CHADEMA)
Ernest Magawe akisoma ripoti yake ya utekelezaji wa majukumu tangu
alipochaguliwa mnamo mwaka 2015 /2020.
Mke wa Diwani wa kata ya Kibamba aliyemaliza
kipindi cha muda wake akitoa neo la shukrani mara baada ya kumalizika kwa
halfa hiyo ya kutoa ripoti ya utekelezaji wa majukumu yake wakati wa kipindi
chake cha uongozi kuanzia mwaka 2015 hadi 2020.
Na Victor Masangu, Kibamba
Diwani wa kata ya Kibamba aliyemaliza muda wake wa kuongoza
kwa mipindi cha miaka mitano kupitia tiketi ya Chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) Ernest
Mgawe amekabidhi ripoti maalumu kwa uongozi wa chama chake ambayo imetaja vipaumbele 14 vya msingi ambayo amevitekeleza
wakati wa uongozi wake kuanzia kipindi
cha mwaka 2015/2020 katika sekta mbali mbali ikiwemo afya, elimu, maji pamoja na miundombinu ya barabara.
Akizungumza katika halfa fupi ambayo iliandaliwa kwa ajili
ya kukabidhi ripoti hiyo kwa uongozi wa chama ngazi ya Wilaya pamoja na
viongozi wengine waandamizi kutokea kwenye mitaa mbali mbali alisema kwamba
ripoti ndani ya ripoti hiyo imeweza kuelezea mambo mbali mbali ya kimaendeleo
ambayo yalifanyika katika kipindi cha miaka mitano iliyopita tangu kuchaguliwa
kwake.
Mgawe alibainisha kwamba anamshukuru mwenyezi Mungu kwa
kuweza kumsaidia katika kutekeleza majukumu yake katika kipindi chote kwa
kushirikiana bega kwa bega na viongozi wake wa chama kwa lengo la kuweza
kuwalatea mabadiliko chanya wananchi wa kata ya kibamba katika Nyanja mbali
mbali lengo ikiwa ni kutimiza zile ahadi ambazo alizitoa kabla ya kuchaguliwa
kwake.
“Katika miaka mitano ya uongozi wangu kuanzia mwaka 2015
hadi mwaka huu wa 20202 tumeweza kwa kweli kushirikiana na wanananchi wa
kibamba katika maeneo mbali mbali na pia nina imani kuwa upendo wao na
ushirikiano wao ambao walinipatia katika kipindi chote ndio umeweza kunifukisha
hapa hadi nimemaliza kipindi changu salama hivyo nina imani siku zote mafanikio
hayawezi kuja pasipo kuwa na kuwa na ushirikiano baina na uongozi pamoja na
wananchi wenyewe.,”alisema Mgawe.
Aidha alisema kuwa wakati wa kipindi chake cha uongozi
aliweza kushiriki kikamilifu katika shughuli mbali mbali za kijamii ikiwemo
kuchangia ujenzi wa nyumba za ibada, sambamba na kutoa misaada mbali mbali
katika kuwasaidia baadhi ya wananchi
katika masuala ya matibabu kwa ambao walikuwa na changamoto ya kutojiweza
katika gharama sambamba na kuwahudumia wajane.
Katika hatua nyingine alisema kwamba katika kuhakikisha
kwamba suala la ulinzi na usalama linaimarishwa kwa wananchi wake na kuondokana
na wimbi la uharifu na unyanganyi alishirikiana kwa dhati na jeshi la Polisi katika kufanikisha ujenzi wa kituo
cha polisi ambacho kilijengwa katika maeneo ya gogoni ambacho kimeweza kusaidia
kwa kiasi kikubwa mambo ya uharifu.
Pia Diwani huyoa aliyemaliza muda wake kalisema kwamba
katika upande wa miundombinu ya barabara kila mwaka anahakikisha barabrara
zinazotumiwa na wananchi wengine zinafanyiwa ukaarabati wa kina ikiwemo
kuziwekea vifusi pamoja na zile nyingine za mitaani kuchongwa ili ziweze
kupitika kwa urahisi hasa katika kipindi cha mvua zinaponyesha.
Diwani huyo alielezea kwamba kulikuwa na changamoto kubwa ya
upatikanaji wa huduma ya maji pindi alipoingia madarakani hivyo aliamua
kushirikiana na wadau wa maendeleo katika kuhakikisha anamaliza kero ya maji
kwa wananchi wa kata ya kibamba hasa katika maeneo ya mtaa wa kibwegere ambao
ulikuwa na shida hiyo lakini kwa sasa serikali imeshatenga bajeti kwa ajili ya
usambazaji wa msji katika maeneo mbali mbali.
Katika kipindi cha kuanzia mwaka 2015 hadi 2020 Diwani huyo
aliyemaliza muda wake aliweza kutekeleza majukumu yake mabali mbali ikiwemo
kuleta huduma bila ya ubaguzi, kushiriki katika shughuli za kijamii,kuwahudumia
wajane,ulinzi na usalama,miuundombinu ya barabara, huduma ya maji,
umeme,ardhi.afya, elimu pamoja mutatua migogoro ndani ya kata.
No comments:
Post a Comment