HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 13, 2020

WATANZANIA ENDELEENI KUFUATA MAELEKEZO YA WATAALAM WA AFYA MAPAMBANO DHIDI YA COVID 19

Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha, David Lyamongi, akiongea wakati akipokea msaada wa Ndoo za kunawia mikono zilizotolewa na Umoja wa waalimu wakuu  Tahossa  kwa ajili ya kuendelea kujikinga na maambukizi ya ugonjwa wa homa kali ya mapafu Covid 19 leo jijini Arusha 

Katibu Mkuu wa Umoja wa Waalimu Wakuu wa shule mkoa wa Arusha (Tahossa), akizungumza wakati wa makabidhiano ya vifaa vya kujikinga na maambukizi ya ugonjwa wa homa kali ya mapafu Covid 19 vilivyotolewa na umoja huo leo kwenye ofisi za mkuu wa mkoa wa Arusha.

Sehemu ya Ndoo 25 zilizotolewa na umoja wa Waalim wakuu leo jijini Arusha ikiwa ni muendelezo wa kuisaidia serikali kwenye mapambano ya ugonjwa wa covid 19 unaosababishwa na virusi vya corona.
Kaimu Katibu tawala wa Mkoa wa Arusha akikabidhiwa vifaa hivyo na uongozi wa umoja wa waalimu wakuu Tahossa mkoa wa Arusha.
Picha ya pamoja mara baada ya makabidhiano hayo leo jijini Arusha kwenye Hafla iliyofanyika kwenye ofisi ya mkuu wa mkoa wa Arusha.



 Arusha, Tanzania.


Watanzania wameaswa kuendelea kuchukuwa hatua dhidi ya maambukizi ya Ugonjwa wa homa kali ya mapafu(covid 19) kwa kuendelea kufuata maelekezo ya wataalam wa Afya nchini kwa lengo la kupambana na maambukizi mapya.


Kauli hiyo imetolewa na kaimu katibu tawala mkoa wa Arusha David Lyamongi kwenye hafla ya makabidhiano ya vifaa vya kujikinga na maambukizi ya ugonjwa wa Covid 19 unaosababishwa na virusi vya Corona kutoka kwa Tahosa mkoa wa Arusha jijini hapa 

Alisema kuwa serikali ya mkoa inaendelea kuwataka wadau wa maendeleo kuendelea kushirikiana nayo kuhakikisha wanaendeleza juhudi za kuutokomeza ugonjwa huo nchini hivyo msaada huo utaendeleza mapambano ya kukabiliana nao.

Akawataka waalimu kuendelea kushirikiana na serikali katika kuongeza juhudi za kuondokana na changamoto ya Maradhi hayo kwa kuendelea kuwa mabalozi wa kuhamasisha mapambano ya ugonjwa huo.

"Niwasihi sana waalimu toeni elimu ya usafi kwa jamii yetu inayowazunguka kuondoa changamoto za magonjwa ya milipuko kwani Elimu inafaa sana na  itasaidia jamii yetu kuwa na uelewa siku za usoni kuondokana na maradhi au kujikinga nayo"

Awali akiongea kwenye hafla hiyo iliyofanyika kwenye ofisi ya mkuu wa mkoa wa Arusha Afisa Elimu Taaluma mkoa wa Arusha Joseph Ngoseki alisema kuwa umoja huo walionyesha waalimu hao uendelezwe ili kuendelea kushirikiana na serikali kupambana na janga la corona.

Kwa Upande wake Katibu wa umoja wa wakuu wa shule Tahosa mkoa wa Arusha Mwalim Victor Mbwambo alisema kuwa Ndoo hizo 25 walizokabidhi leo zimelenga kusaidia mapambano dhidi ya ugonjwa wa Covid 19 na mkoa utapanga sehemu watakayoona inafaa.

Alisema kuwa msaada huo umelenga kuisadia serikali katika kupambana na ugonjwa wa homa kali ya mapafu Covid 19 na waliangalia vifaa hivyo mfano vitakasa mikono barakoa lakini wakaona ndoo zitakuwa na msaada mkubwa kwani hata kama hakutakuwa na maambukizi mapya itasaidia kuwaweka safi ili kuepuka magonjwa.

No comments:

Post a Comment

Pages