HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 13, 2020

MBUNGE CATHERINE MAGIGE AZITAKA SHULE KUONGEZA UFAULU KWA VIJANA MASOMO YA TEHAMA

Sehemu ya vifaa vya Tehama vilivyotolewa na Mbunge wa viti maalum mkoa wa Arusha Catherine Maggige kwa shule Tatu za sekondari za Makiba Nanja na Ngaranaibo zilizopo kwenye wilaya za Arumeru Monduli na Longido mkoani Arusha vifaa hivyo vyenye thamani ya milion 38 ikiwa ni kuboresha elimu ya tehama na kuongeza Ufaulu kwa wanafunzi wa mkoa huo katika hafla iliyofanyika katika ukumbi wa mkuu wa mkoa wa Arusha leo jijini Arusha. (Picha na Ahmed Mahmoud Arusha).
Baadhi ya waalimu wa shule za Makiba Ngaranaibo na Nanja wakifuatilia hafla hiyo ya makabidhiano kwenye ukumbi wa Ofisi ya mkuu wa mkoa wa Arusha leo jijini hapa.
Waalimu wakuu wa shule za sekondari wakifuatilia hafla ya kupokea vifaa vya Tehama kutoka kwa Mgeni Rasmi Kaimu KaTawala mkoa wa Arusha David Lyamongi hayupo pichani Leo jijini Arusha katika Ukumbi wa Mkuu wa Mkoa wa Arusha.
Afisa Elimu Taaluma mkoa wa Arusha Joseph Ngoseki akiongea kwenye Hafla ya kukabidhi vifaa vya Tehama kwa shule tatu zaSekondari za mkoa wa Arusha zilizopo kwenye wilaya Tatu za Monduli, Longido na Meru jijini Arusha.


Na Ahmed Mahmoud, Arusha

Mbunge wa viti maalum mkoa wa Arusha Catherine Maggige Amezitaka shule mkoani Arusha kuhakikisha wanaongeza ufaulu kwa wanafunzi ikiwemo masomo ya tehama kwa kuwa dunia inaelekea kwenye teknolojia hiyo ya mawasiliano kwa sasa.


Maggige ameyasema hayo kwenye hafla ya kukabidhi vifaa vya tehama zikiwemo Kompyuta 25 na mashine za kudurufu vyenye thamani ya milion 38 aliyowakilishwa na mratibu wake Philip Amoh kwa shule tatu za Ngarnaibo Makiba na Nanja zilizopo kwenye wilaya za Arumeru,Monduli na
Longido mkoani Arusha.


Alisema kuwa Msingi huo utasaidia sana kuongea uelewa wa elimu mtandao na kuwasaidia vijana wa mkoa wa Arusha kuongeza maarifa zaidi yatakayosaidia kwenda na teknolojia hiyo ya mawasiliano.
 

"Wakuu wa shule na maafisa elimu hakikisheni mnavisimamia vyema vifaa hivi kwa lengo la kuongeza wigo mpana wa ufaulu kwa vijana wetu na tukiona matumizi yameenda kama malengo yalivyo kusudiwa tutaweza
kuongeza nawashukuru sana mfuko wa fursa sawa kwa wote kwa kushirikiana nami kutoa msaada huu wenye thamani ya milion 32"
 

Kwa Upande Kaimu Katibu tawala wa mkoa wa Arusha David Lyamongi alisema kuwa vifaa hivyo mashine za vidurufu na kompyuta vitasaidia kuboresha elimu ya teknolojia ya mawasiliano kwa shule zetu na kuwataka wote waliopewa kwenda kuvitumia kwa malengo yaliokusudiwa.

Alisema kuwa ongezeko la vifaa hivyo kwa shule zetu mkoani Arusha kwa ujumla vimesaidia kuongeza ufaulu kwa wanafunzi hivyo kuendelea kumpongeza mbunge huyo kwa kuendelea kushirikiana na serikali ya mkoa kukuza elimu kwa vijana wetu mashuleni.


"Naomba nitumie fursa hii kumpongeza mbunge Catherine kwa kuwa amekuwa mstari wa mbele na msaada kwetu kwa muda mrefu ametutetea na kusaidia serikali kwenye shughuli mbalimbali za kijamii katika mkoa naomba

No comments:

Post a Comment

Pages