HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 19, 2020

KYERWA KUANZA ZOEZI LA KUHAKIKI DAFTARI LA WAPIGA KURA

Na Lydia Lugakila, Kagera
 
Wilaya ya Kyerwa mkoani Kagera inatarajia kuanza zoezi la
uhakiki wa daftari la mpiga kura kwa awamu ya pili na ya
mwisho kuanzia Juni 17 hadi 20 mwaka huu.
 
Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Kyerwa Shadrack Muagama katika kikao maalum kilichofanyika katika ukumbi wa wilaya hiyo ambapo ameeleza kuwa Daftrai hilo la wapiga kura litawekwa wazi katika vituo walivyojiandikisha wananchi hao.

Muagama amewasisitiza Watendaji wa vijiji kuhakikisha
wanasimamia zoezi hilo kwa ufasaha.

Aidha mkurugenzi huyo amesema kuwa marekebisho ya
mwisho yatampasa mwananchi kwenda katika wilaya hiyo pale zitakapojitokeza changamoto ikiwemo majina kutokuwa sahihi au picha kutotoka kwa usahihi.
 
Hata hivyo Muagama amesema kuwa wananchi hao
wanapaswa kutosubiri kwenda siku ya mwisho kufanya uhakiki badala yake waanze kwa wakati na kumaliza kwa wakati.

No comments:

Post a Comment

Pages