Mkuu
wa Wilaya ya Nzega Godfrey Ngupula akitoa ufafanuzi jana kwa Watendaji
wa Vijiji na Kata wakati walipokuwa wakielezwa umuhimu wao kusimamia
zoezi la ugawaji wa Vitambulisho vya Wajasiriamali.
Kaimu
Meneja wa Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) Mkoani Tabora Aniseti Antony
akieleza jana wilayani Nzega aina ya wafanyabiashara wadogo ambapo
wanapaswa kuchukua vitambulisho.
NA TIGANYA VINCENT
SERIKALI Mkoani Tabora inachunguza
tuhuma dhidi ya baadhi ya Mawakala wa Benki
ambao wanakataa kupokea fedha za vitambulisho vya wajasiriamali wadogo
kwa madai hawapati faida.
Kauli hiyo imetolewa jana
wilayani Nzega na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri baada ya kupata
malalamiko kutoka kwa Watendaji kuwa Mawakala wa Benki wanakata kupokea fedha
zinakusanywa kutoka kwa Wajasiriamali wadogo.
Alisema wakiwabaini
Mawakala ambao wamekataa kupokea fedha itawasaliana na Benki husika ili ziweze
kuchukua hatua dhidi ya Mawakala hao.
Mwanri alisema kuwa
maelekezo ya Seikali yako wazi kuwa fedha zote zitalipwa kwa kutumia Control
Number kupitia Wakala wa Benki au Benki na sio vingine.
Alisema watakaobainika
kuwa wanaokataa kupokea fedha kwa madai hawapati faida watahesabiwa kuwa wanahujumu
jitihada za Serikali na watachukuliwa hatua ili iwe fundisho kwa wengine.
Mkuu huyo wa Mkoa aliongeza
hairusiwi Watu wote waliopewa jukumu la kugawa vitambulisho kwa wajasiriamali
wadogo kutumia fedha kwa kutumia mitandao ya simu.
Alisema kufanya hivyo
kutasababishia Serikali kupata fedha pungufu ya gharama halisi ya kitambulisho
na hivyo kuzalisha hoja.
Kwa upande wa Kaimu
Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoani Tabora Aniseti Antony alisema
Mamlaka hiyo ina mkataba ya Benki , hivyo inasikitishwa na kitendo cha Wakala
wao kukata kupokea fedha za vitambulisho.
Alisema Serikali ina
utaratibu wake wa kuzilipa Benki . hivyo Mawakala hawapaswi kugoma kupokea
fedha za Vitambulisho.
Antony alisema watajitahidi
kuwasiliana na Benki husika ili kuhakikisha zoezi hilo halikwami na kusababisha
Watendaji kukaa na fedha za umma kwa muda mrefu bila kuziwasilisha Benki.
No comments:
Post a Comment