Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri akitoa elimu leo kwa Wafanyabiashara wadogo wa Puge wilaya Nzega juu ya umuhimu wa kuchukua vitambulisho vya Wajasiriamali. (Picha na Tiganya Vincenti).
NA TIGANYA VINCENT
SERIKALI imesema
itawachukulia hatua Watendaji ambao wataobainika kuzungusha fedha za
vitambulisho vya Wajasiriamali wadogo kwa nia ya kutaka kuzalisha faida kabla
ya kuzikabidhi Benki.
Kauli hiyo imetolewa jana
wilayani Igunga na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri wakati akiendesha zoezi
la kuwahamasisha wajasirimali kuchukua vitambulisho vipya vilivyotolewa hivi
karibuni na Serikali.
Alisema kuna tabia ya
baadhi ya Watendaji wanaweza kukusanya fedha za vitambulisho na kuzipangia
matumizi yao binafsi kwa lengo kuwa wakishazalishi ndio wapeleke Benki.
“Ni marufuku kutumia
fedha za viparata ili kuzungushia kwenye biashara zenu mnaweza kupoteza fedha
za umma na kujikuta katika matatizo…mkichukua fedha hizo mkaenda kununua
ng’ombe au mkanunua mpunga kwa lengo la kutaka kuzalisha mtajikuta mnajiingiza
katika matatizo na kushitakiwa na kufukuzwa kazi” alisisitiza.
Mwanri alisema Mtendaji
yoyote atakayekuwa ametumia fedha hizo atahesabika kuwa mwizi na kupelekwa
Mahakamani kwa kosa la wizi wa fedha za umma.
Naye Kaimu Maneja wa
Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) Mkoani Aniseti Antony alisema matumizi ya fedha
za umma yanautaratibu wake.
Alisema ni marufuku
kutumia fedha za umma kabla ya kuidhinishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania.
No comments:
Post a Comment