Mrisho Gambo |
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John
Pombe Magufuli leo tarehe 19 Juni, 2020 ametengua uteuzi wa viongozi 3 wa Mkoa
wa Arusha na kufanya uteuzi wa viongozi watakaoshika nyadhifa hizo.
Kwanza,
Mhe. Rais Magufuli ametengua uteuzi wa Mkuu wa Mkoa wa Arusha Bw. Mrisho Gambo
na amemteua Bw. Idd Kimanta kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha.
Kabla ya uteuzi huo Bw. Kimanta alikuwa Mkuu wa Wilaya
ya Monduli Mkoani Arusha. Nafasi ya Mkuu wa Wilaya ya Monduli itajazwa baadaye.
Pili,
Mhe. Rais Magufuli ametengua uteuzi wa Mkuu wa Wilaya ya Arusha Bw. Gabriel
Daqarro na amemteua Bw. Kenan Kihongosi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Arusha.
Kabla ya uteuzi huo, Bw. Kihongosi alikuwa Mwenyekiti
wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Iringa.
Tatu,
Mhe. Rais Magufuli ametengua uteuzi wa Mkurugenzi Halmashauri ya Jiji la Arusha
Dkt. Maulid Madeni na amemteua Dkt. John Pima kuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya
Jiji la Arusha.
Kabla ya uteuzi huo, Dkt. Pima alikuwa Mkurugenzi wa
Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua Mkoani Tabora.
Aidha, Mhe. Rais Magufuli amemteua Bw. Jerry Mwaga kuwa
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua. Kabla ya uteuzi huo Bw. Mwaga
alikuwa Afisa katika Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).
Wateule wote wanatakiwa kuwepo Ikulu Jijini Dar es
Salaam, Jumatatu tarehe 22 Juni, 2020 saa 2:30 asubuhi.
No comments:
Post a Comment