NA TIGANYA VINCENT
MKUU
wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri, ametoa mwezi mmoja kwa viongozi wa
Halmashauri zote kuhakikisha wamemaliza kugawa vitambulisho vya
wajasiriamali ambavyo vimetolewa hivi karibuni.
Alisema
hakuna sababu ya kuchukua muda mrefu katika ugawaji wa vitambulisho
hivyo kwa sababu wameshapata uzoefu kutokana na vile vya mwaka jana.
Mwanri
alitoa kauli hiyo jana mjini Igunga wakati wa mkutano wake na Watendaji
wa Kata na Vijiji kuhusu umuhimu wa kutekeleza zoezi hilo.
Alisema
uendaji wa Mtendaji yoyote utapimwa pamoja na majukumu mengine ni
pamoja na jinsi aakavyofanikisha zoezi la kuwezesha wajasirimali wadogo
na watoa huduma kuchukua vitambukusho
Aidha
Mwanri aliongeza kuwa kila watakapokuwa wakiuza kitambulisho
wahakikishe fedha wanazipeleka benki au wanalipa kwa wakala wa Benki kwa
kutumia Control namba.
Katika
hatua nyingine Mkuu huyo wa Mkoa ametahadharisha Waendaji kuwa makini
kabla ya kutoa vitambulisho kwa kupata taarifa sahihi ya mhusika ili
kuhakikisha wanaopatiwa ni walengwa tu na sio wafanyabiashara wakubwa.
Alisema
kuna uwezekano wa Wafanyabiashara wakubwa wakatumia wafanyabiashara
wadogo kuchukua vitambulisho hivyo kwa ajili ya kukwepa kodi.
No comments:
Post a Comment