HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 01, 2020

WIZARA YA MIFUGO YATOA VITENDEAKAZI KUBORESHA UCHUNAJI WA NGOZI

Mkurugenzi wa Uzalishaji na Masoko wizara ya Mifugo na Uvuvi Felix Nandonde, akimkabidhi vifaa vya uchunaji wa ngozi kwenye machinjio ya mkoa wa Arusha kwa ajili ya kuboresha Uzalishaji wa Ngozi Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa huo, David Lyamongi, kwenye hafla iliyofanyika kwenye ofisi za mkuu wa mkoa huo jijini Arusha. (Picha na Ahmed Mahmoud, Arusha).


Na Ahmed Mahmoud, Arusha
 
Wizara ya mifugo na uvuvi imetoa vitendeakazi vya mazao ya mifugo kwa wachunaji wa ngozi kwenye machiinjio yote ya mkoa wa Arusha kwa ajili ya kuongeza thamani na kuboresha uchunaji wa Ngozi.

Akikabidhi vifaa hivyo kwa Kaimu Katibu Tawala wa mkoa wa Arusha kwa niaba ya wachunaji hao Mkurugenzi wa masoko na uzalishaji Felix Nandonde alisema kuwa kwa kipindi kirefu ngozi zimekuwa  zikiharibiwa ubora wake kwa matumizi ya vifaa visivyo na ubora.

kwa mujibu wa Nandonde wizara ilitoa mafunzo ya siku moja kwa wachunaji wa ngozi mkoa wa Arusha ili kuboresha thamani ya Ngozi ikiwemo kutoa leseni kwa kila mchunaji na vifaa hivyo kwa lengo la kuongeza ubora kwenye kazi zao.

Alivitaja vitendea kazi hivyo kuwa visu vya kisasa ambavyo
vimetengezwa kwa teknolojia ya kisasa na vitatolewa bora kwa wachunaji wa mkoa wa Arusha na nchini kwa ujumla

“Kwa kipindi kirefu sekta ya uchunaji nchini imekuwa ikionekana haina mwenyewe lakini sasa kupitia serikali ya awamu ya tano imeanza kutambulika kwa lengo la kuongeza mnyororo wa thamani wa mazao ya mifugo”

Akiongea mara baada ya kupokea vifaa hivyo kaimu katibu tawala wa mkoa wa Arusha David Lyamongi aliipongeza wizara hiyo kwa kutoa mafunzo kwa wachunaji pamoja na vitendeakazi hivyo.

Aliongeza kuwa vitendeakazi hivyo vitawezesha mkoa huo kuzalisha ngozi zenye ubora wa hali ya juu na hivyo ngozi zitakuwa na thamani kubwa na masoko ya hali ya Juu.

Alisema kuwa mkoa wa Arusha ambao ni wa wafugaji vifaa hivyo vimekuja wakati muafaka kusaidia kuondokana na matumizi ya vifaa butu ambavyo vilikuwa vikitumika kuharibu ubora wa Ngozi na hivyo kuondoa thamani
yake.

No comments:

Post a Comment

Pages