Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey
Mwanri(katikati) akikabidhi jana mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi
milioni 140 kwa vikundi mbalimbali vya Halmashauri ya Mji wa Nzega. (Picha na Tiganya Vincent).
NA TIGANYA VINCENT
UONGOZI wa Halmashauri
ya Wilaya ya Nzega umeagizwa kukata katika mishahara watumishi wanaodaiwa
masurufi ya kiasi cha shilingi milioni 10.3 yaliyosababisha hoja ya kiukaguzi kutoka
kwa Mdhibiti wa Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).
Agizo hilo Mkuu wa Mkoa
wa Tabora, Aggrey Mwanri, ameagiza kuwakata mishahara watumishi wote wa
alilitoa wakati wa kikao maalumu cha Baraza la Madiwani la Halmashauri hiyo la
kupitia hoja ya mbalimbali kutoka ripoti ya ukaguzi ya CAG kwa mwaka 2018/19.
Alisema ndani ya mwezi
mmoja watumishi wote wanaodaiwa wahakikishe wamelipa fedha hizo au wakatwe
kwenye mishahara yao.
Mwanri alisema wasipo
katwa fedha hizo hoja hiyo itaendelea kujitokeza na kuchafua hesabu za Halmashauri
hiyo wakati wa ukaguzi wa CAG.
Aliwataka Wakuu wa Idara kuhakikisha wamefanyia kazi
hoja zote za CAG na kuwalisilisha vielelezo ili ziweze kufungwa.
Alisema watumishi ni vema wakajitahidi kuzuia
hoja na zio kutoa maamuzi ambayo yanasababisha kuendelea kuzalisha hoja kila
mwaka.
Katika hatua nyingine Mkuu wa Mkoa amemwagiza
Katibu Tawala Msaidizi(Serikali za Mitaa) kushirikiana na Mkurugenzi Mtendaji ,
Meneja wa RUWASA kuhakikisha wanaibana Drilling Ltd irejeshe shilingi milioni
23.5 baada ya kuchimba visima ambavyo havikuwahi kutoa maji.
Alisema fedha hizo zilipaswa
kuwa zimerejeshwa tangu mwaka jana mwezi Septemba ambapo hadi hivi sasa hakuna
fedha zilizorejeshwa na kuongeza kuwa ikiwa itashindwa kurejesha waipeleke
Mahakamani.
No comments:
Post a Comment