Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri
akizungumza na Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Nzega wakati wa kikao
cha kupitia taarifa ya ukaguzi kutoka katika Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu
wa Hesabu za Serikali (CAG).
NA TIGANYA VINCENT
HALMASHAURI ya Mji wa Nzega imetoa jumla ya shilingi
milioni 140 kwa vikundi 40 ikiwa ni sehemu ya asilimia 10 ya mapato ya ndani.
Mikopo hiyo imekabidhiwa
kwa vikundi hivyo katika halfa fupi ilifanyika jana mjini Nzega.
Akizungumza wakati wa
kukabidhi, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Philemon Magesa alisema kuwa
vikundi 24 vya wanawake vimepatiwa mikopo ya shilingi milioni 74.5.
Aliongeza kuwa kwa upande
wa vikundi 11 vya vijana vimekopeshwa shilingi milioni 38 na vikundi 5 vya watu
wenye ulemavu vimekopeshwa shilingi milioni 27.5.
Wakati huo huo Magesa
alisema kuwa katika kipindi cha mwezi Januari mwaka huu walitoa mikopo ya
shilingi milioni 70 kwa vikundi mbalimbali.
Akizungumza baada ya
kukabidhi mikopo hiyo kwa niaba ya Halmashauri hiyo, Mkuu wa Mkoa Aggrey Mwanri
aliutaka uongozi wa Halmashauri hiyo kuhakikisha wanatoa elimu ya kutosha kwa
wakopaji ili waweze kutambua umuhimu wa kurejesha fedha hizo kwa wakati.
Alisema hatua hiyo
itavisaidia vikundi kutumia fedha kwa malengo waliyoombea na sio katika
shughuli nyingine ikiwemo starehe na kuwafanya washindwe kulipa kwa wakati.
Mwanri alisema hatua hiyo
itawasaidia kuepuka kuwa na wadaiwa ambao wanawasababisha kupata hoja za
Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG) ambazo zinatokana na fedha ambazo
hazijarejeshwa.
Aidha Mkuu wa Mkoa
aliushauri uongozi wa Halmashauri hiyo kuangalia uwezekano wa kuvikopesha
vikundi vifaa vitakavyosaidia kuanzisha viwanda vidogo vodogo.
Katika hatua nyingine
Mkuu wa Mkoa huyo ameagiza uongozi wa Halmashauri ya Mji wa Nzega kuhakikisha
milioni 22.6 zilizokopeshwa katika vikundi mbalimbali zinarejeshwa ili kufuta
hoja za kiukaguzi.
Alisema ni vema
wakasaliana na wahusika ili waonyeshe mpango wao wa kulipa deni na wakishindwa
kurejesha kwa hiari wahakikishe wanapeleka Mahakamani
No comments:
Post a Comment