Katibu Mkuu Wizara ya
Kilimo Ndugu Gerald M. Kusaya
anawatangazia wanachuo na wakufunzi kuwa Vyuo vya Mafunzo ya Kilimo (MATI) vimefunguliwa
rasmi tarehe 01 Juni, 2020 kufuatia
agizo la Mhe. Rais Dkt. John Pombe
Magufuli alilotoa tarehe 21 Mei, 2020.
Wanafunzi wote wa Vyuo vya
Mafunzo ya Kilimo nchini wanatakiwa kuendelea kuripoti vyuoni kwa ajili ya
kuendelea na masomo yao.
Wizara
inawataka wanafunzi wote kuhakikisha wanakuwepo vyuoni ifikiapo tarehe 08 Juni,
2020 na itakapofika tarehe 10 Juni, 2020 Wakuu wa Vyuo vyote wachukue hatua za
kinidhamu na kitaaluma kwa wanafunzi ambao watakuwa hawajaripoti vyuoni.
Aidha, Wakuu wa Vyuo vyote vya Kilimo wanatakiwa wafanye maboresho ya kalenda
ya masomo kwa kuzingatia maagizo ya Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE)
yaliyotolewa tarehe 22 Mei, 2020
Wizara ya Kilimo inasisitiza
kuwa watumishi na wanafunzi wote vyuoni waendelee kuzingatia kanuni zote za
kujikinga na ugonjwa wa homa kali ya mapafu (COVID -19) kama zilivyotolewa
katika mwongozo wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.
Katika hatua
nyingine, Katibu Mkuu ameelekeza wazabuni wote wanaotoa huduma ya chakula vyuoni,
waendelee kutoa huduma hiyo ili kuhakikisha chakula kinapatikana muda ambao
wanafunzi watakuwa wakiendelea na masomo yao.
Imetolewa na;
Kitengo
cha Mawasiliano Serikalini,
Wizara
ya Kilimo
DODOMA
05 Juni,
2020
No comments:
Post a Comment