NA FRANCIS DANDE
KAMPUNI
ya mawasiliano ya simu za mkononi ya Halotel kupitia huduma zake za
kifedha za HaloPesa imejipanga kutoa gawio kwa wateja wake.
Hatua
hiyo ikiwa ni hatua ya kwanza kwa HaloPesa kutoa gawio kiasi cha
shilingi Bilioni moja kwa wateja wake Zaidi ya Milioni 1.9 ambao ni
pamoja na wateja binafsi, mawakala na washirika wake mbalimbali
wanatumia huduma za HaloPesa.
Akizungumza
na waandishi wa Habari Mkuu wa kitengo cha biashara cha HaloPesa,
Magesa Wandwi alisema “Wateja watapata sehemu ya gawio hilo
linalotokana na faida iliyozalishwa kutoka katika akaunti za HalotePesa
Trust zilizoko katika mabenki mbalimbali nchini kati ya Oktoba 2016 na
Desemba 2018.
Wandwi
alisema kuwa faida hiyo ni haki ya wateja na hivyo HaloPesa tunashauku
na furaha kubwa ya kuwalipa wateja wetu gawio hilo kwa mujibu wa sheria ,
kanuni na miongozo mbalimbali toka Benki kuu ya Tanzania (BOT).
“Gawio
hili ni la kwanza kwa wateja wetu na litatolewa ndani ya mwezi mmoja
toka sasa, kiasi cha gawio ambacho mteja wa Halopesa atakipata anaweza
kutumia atakavyo ikiwa ni pamoja na kutoa au kufanya miamala mbalimbali,
alisema na kuongeza
“Tunapenda
kuwasihi wateja wetu kuwa Halotel tunaendelea na kutoa huduma bora
zenye gharama nafuu nchi nzima na waendelee kutumia huduma zetu za
HaloPesa,” alisema Wandwi.
Mkuu wa Kitengo cha Biashara cha HaloPesa, Magesa Wandwi, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Juni 1, 2020 kuhusu kuanza kutoa gawio kwa wateja wake.
Katika muendelezo wa kutoa huduma bora za kifedha nchini.
No comments:
Post a Comment