Baadhi
ya Nchi za Ulaya zimeanza kutambua na kupongeza hatua ambazo Tanzania
imezichukua katika kupambana na Virusi vya Corona vinavyosababisha
ugonjwa wa COVID 19 kutokana na muongozo wa Rais Dkt John Pombe Magufuli
kwa kuwa zinaendana mazingira na hali halisi ya Tanzania.
Waziri
wa Maendeleo ya Kimataifa wa Norway Bw. Dag-IngeUlstein ametoa pongezi
hizo na kutambua jitihada za Rais Dkt John Pombe Magufuli za kutoweka
zuio kwa watanzania kutotoka nje (lockdown) kama nchi nyingi duniani
zilivyofanya huku tahadhari ikitolewa kwa wananchi kujikinga na kufuata
muongozo wa wataalam wa afya jambo ambalo limeifanya Tanzania
kutoathirika kwa kiasi kikubwa na ugonjwa huo.
Ameongeza
kuwa ni Dhahiri kuwa ugonjwa wa COVID 19 ni ugonjwa mpya ulimwenguni
ambao kila nchi imechukua hatua na afua ambazo zinaendana na hali
halisi,mazingira ya nchi husika na kupongeza msimamo wa Tanzania na
hatua zinazoendelea kuchukuliwa katika kupambana na ugonjwa huo ikiwa ni
pamoja na kutoa tahadhari kwa wananchi kufuata muongozo wa wataalam wa
afya.
Kwa
upande wake Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Prof. Palamagamba John Kabudi amemshukuru Waziri huyo wa Norway kwa
kutambua jitihada za Tanzania katika kupambana na virusi vya corona
licha ya baadhi ya nchi kubeza muongozo wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli
wa kuweka zuio la kutoka nje (lockdown).
Pia
ameishukuru Norway kwa kuahidi kuendelea kushirikiana na Tanzania
katika masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja na masuala ya kidiplomasia na
maendeleo hususani katika kusaidia jitihada za kupambana na mabadiliko
ya tabianchi na kuhakikisha kuwa Tanzania inafikia malengo yake katika
utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu.
Mazungumzo
baina ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Prof. Palamagamba John Kabudi na Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa wa
Norway Bw. Dag-IngeUlstein yamefanyika katika Ofisi za Wizara za Jijini
Dodoma kwa lengo la kuimairisha mahusiano baina ya nchi hizo pamoja na
kubadilishana uzoefu katika kupamabana na virusi vya corona.
Waziri
wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba
John Kabudi (Mb) akizungumza na Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa wa
Norway Bw. Dag-IngeUlstein. Mazungumzo
hayo yamefanyika kwa njia ya mtandao(video confrencing) katika ofisi
za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Jijini Dodoma.
Waziri
wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba
John Kabudi (Mb) akiwa pamoja na baadhi ya watumishi wa Wizara ya Mambo
ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akifuatilia mazungumzo yake na
Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa wa Norway Bw.
Dag-IngeUlstein,mazungumzo yaliyofanyika kwa njia ya mtandao (video
Conferencing) jijini Dodoma.
Waziri
wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba
John Kabudi (Mb) pamoja na baadhi ya watumishi wakiandika kitu wakati wa
mazungumzo na Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa wa Norway Bw.
Dag-IngeUlstein,mazungumzo yaliyofanyika kwa njia ya mtandao (video
Conferencing) jijini Dodoma.
No comments:
Post a Comment