Na Mwandishi Wetu
WAGOMBANAPO
Ndugu shika jembe ukalime, unaweza kueleza hivyo mara baada ya klabu ya
Yanga na Mshambuliaji wao wa kimataifa David Molinga kuonyeshana mabavu
kikosi kikitua mjini Shinyanga kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu Tanzania
Bara.
Kikosi
cha Yanga kiliondoka jana alfajiri na kufanikiwa kutua Shinyanga salama
kuwakabili Mwadui FC ukiwa ni mchezo wa kwanza kutoka kwenye janga la
Virusi vya Corona, ambapo Ligi ilisimama tangu Machi 17 mwaka huu.
Kwa
mujibu wa taarifa za klabu kupitia App yao zilieleza kuwa Molinga
amegoma kusafiri na timu kwa sababu zake binafsi jambo amablo liliukera
uongozi na kuamua kumuacha.
Baaada
ya taarifa hizo kushika kasi Molinga aliibuka na kukanusha taarifa hizo
kupitia ukurasa wake wa Instagram akieleza kuwa hajagoma bali
hakujumuishwa kwenye kikosi kinachoenda kuikabili Mwaduo juni 13.
“Nataka
nikanushe hii habari kwamba nimegoma kusafiri na timu kwanza
nimewakumbushe kitu cha peke imenileta Tanzania ni mpira na kazi yangu
ndio iyo sasa iko ivi tangu timu imeanza mazoezi sijawahi kukosa na
nafata ‘program’ za mwalim vizuri lakin jana orodha ilitoka na mimi jina
langu ajakwepo sasa.
“Itasemekana
vipi mimi nimegoma kama ndio ivyo muulizeni kocha ndio alitajia orodha
yake, imekuwa tabia kila mara kila kitu mimi tu ata kama sjafanya kitu
kibaya utaskia tu molinga ‘this is too much’imezidi sasa.”aliandika
Molinga.
Akizungumza na
Habari Mseto, Ofisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli amesema Molinga
amegoma kusafiri na timu kwa sababu zake binafsi sio kwamba
hajajumuishwa kwenye kikosi.
“Suala
la Molinga niliandika mwenyewe kwe App yetu kwa sababu kilichotokea
chote nilikishuhudia kwa macho yangu sijahadithiwa, yaani nikwamba
wachezaji waliitwa kambini yeye hakuja kwa sababu hakukuwa na
ufuatiliaji tu kajua atakuja.
“Alipopigiwa
simu na Meneja akasema sawa najiandaa mnipitie Shekilango, tumetoka
tumefika Shekilango akapigiwa simu hapokei, Meneja akashuka kwenye gari
akamfuata nyumbani kwake akamgongea akafungua mlango akamwambia bwana
twende akasema siendi sijui siko jina langu sikulisikia jana akaanza
kueleza sababu tofauti na aliyoaeleza mwanzo.
“Kwaiyo
sababu zake ziwe za msimu zisiwe za msingi hata kama anazieleza kwenye
vyombo vya habari ni kwamba amegoma."amesema Bumbuli
Sakata
hilo limechukua nafasi kubwa katika vyombo vya habari kiasi cha kuanza
kuibuliwa hoja nyingine ambazo zinaonyesha kuwa ndani ya Yanga
yawezekana hakuko salama.
Yanga
wanatarajiwa kukata utepe jumamosi hii katika Uwanja wa Kambarage mjini
Shinyanga dhidi ya Mwadui huku wakihitaji matokeo chanya kurudisha
Imani na ari ya mashabiki baada ya kutoka kupoteza mchezo wa kirafiki
dhidi ya KMC FC walipolala kwa mabao 3-0. Uwanja wa uhuru jijini Dar es
Salaam.
No comments:
Post a Comment