Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo,
akizungumza katika mkutano wa kikao kazi na maofisa Tarafa, waatendaji wa kata,
watendaji wa vijiji pamoja na wenyeviti wa vijiji uliofanyika katika ukumbi wa
shule ya sekondari Minaki (Picha na Victor Masangu).
Victor Masangu, Kisarawe
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo amekemea vikali
sakata la vitendo vya utoro,mimba za utotoni pamoja na suala la ubakaji kwa watoto wadogo vinavyofanywa na
baadhi ya watu wazima kinyume kabisa na sheria na taratibu
za nchi kwani vinachangia kwa kiasi kikubwa kukatisha ndoto za watoto hao ambao
wamezipanga katika maisha
yao na kutaka watu
kama hao wawajibishwe na chukuliwe
hatua.
Kauli ya Jokate ameitoa
wakati wa ufunguzi rasmi wa mkutano wa
kikao kazi kati ya Mkurugenzi mtendaji
wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe ambao ulizijumuisha kata zote 17 ambazo
ziliwakilishwa na Maofisa Tarafa, watendaji wa kata, watendaji wa vijiji pamoja
na wenyeviti wa vijiji vipatavyo 84 kwa lengo la kujadili miradi mbali mbali ya maendeleo na kuwataka wenyeviti na
watendaji kuacha tabia ya kugombana na badala yake wajadili changamoto
zinazowakabili.
"Kwa weli mkutano huu ni muhimu sana katika suala zima
la kuleta maendeleo kwa wananchi wetu wa Wilaya ya Kisarawe, kwani tumeweza
kuwakutanisha maofisa tarafa,watendaji wa kata, watendaji wa vijiji pamoja na
wenyeviti mbali mbali wa vijiji,hivyo ninawaomba masuala mbali mbali yote
ambayo tutayajadili hapa ni lazima tuyafanyie kazi hasa hii changamoto ya
watoto wetu kufanyiwa vitendo vya ubakaji na watu wazima na wengine kujikuta
wanakatisha masomo yao ni vema tukashirikiana kuanzia ngazi za chili ili
kulitafutia ufumbuzi suala hili,"alisema Jokate.
Aidha Mkuu huyo alisema kwamba serikali ya awamu ya tano
lengo lake kubwa ni kuhakikisha inawaltea wananchi maendeleo ikiwemo kutoa
elimu bora, hivyo hawezi kulifutia
mamcho sualo la watoto kutokana na vitendo wanavyofanyiwa na
kuwataka wale wote ambao watabainika kuhusika wakamatwe na kuchukuliwa hatua
kali za kisheria ili iwe
fundisho kwa wengine wenye tabia kama hivyo.
Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya
ya Kisarawe Mussa Gama amesema kwamba lengo la kuwakutanisha viongozi na
wawatendaji hao ni kufanya
tatmini ya utekelezaji wa majukumu ya kusimamia miradi mbali
mbali ya maendeleo katika ngazi husika,ambapo pia ameahidi kuvalia njuga maagizo yote ambayo yametolewa
na Mkuu wa Wilaya hasa suala la watoto wadogo kubakwa.
Gama alibainisha kuwa katika kikao kazi hicho kimeweza
kuweka mipango mikakati kwa viongozi na watendaji katika kuhakikisha
wanatekeleza majukumu yao ipasavyo, ikiwemo
katika masuala ya kusimamia utekelezaji wa miradi mbali
mbali ya maendeleo sambamba na kufanya kazi kwa weledi na kuwatumikia wananchi
wao kwa hali na mali lengo ikiwa
ni kuleta mabadiliko chanya ya kimaendeleo,"alisema
Gama.
"Mimi kama
mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe nimeamua kuwakutanisha
viongozi mbali mbali wakiwemo maofisa tarafa, watendaji wa kata, watendaji
wa vijiji, pamoja na wenyeviti wa vijiji vipatavyo 84 ili
kujadili changamoto zinazowakabili na kuzitafutia ufumbuzi wa kudumu sambamba
na kuwajengea uwezo katika suala zima la ukusanyaji wa mapato na utunzaji wa
mazingira, afya, elimu na kujengewa uwezo sheria ambazo zinatumika katika
majukumu yao ya kila siku,"alisema Gama.
Nao baadhi ya wenyeviti na watendaji ambao walihudhuria katika kikao kazi hicho cha kazi akiwemo
Mwenyekiti wa mji mdogo Ally Mkomwa na Mariamu Kimbeo mwenyekiti wa kijiji cha
kikwete wamekiri kuwepo kwa changamoto
ya baadhi ya wanafunzi kukatisha masomo yao kutokana na kupata ujauzito pamoja
na baadhi ya watu kuwabaka watoto wadogo
hali ambayo wamedai inaruudisha
nyuma maendeleo ya sekta ya elimu hivyo
jambo hilo watakwenda kulisimamia vilivyo ili kukomesha kabisa hali hiyo.
HALMASHAURI ya Wilaya ya Kisarawe iliyopo katika Mkoa wa
Pwani licha ya kupiga hatua za kimaendeleo katika baadhi ya sekta lakini bado
imekuwa ikikabiliwa na ngamoto ya watoto
kukatisha masomo yao, wengine kupata mimba za utotoni, vitendo vya ubakaji kwa
watoto wadogo ,hivyo kunahitajika juhudi za makusudi kutoka kwa serikali na
wadau ili kukomesha hali hiyo.
No comments:
Post a Comment