Kikosi cha Yanga.
Na Mwandishi Wetu
KISASI
juu ya kisasi unaweza ukasema kwenye mchezo wa leo kati Mabingwa wa
Kihistoria wa Ligi Kuu Bara (VPL), Yanga SC dhidi ya Kagera Sugar ‘Wana
Nkurukumbi’ utakaopigwa saa 1 jioni, Uwanja wa Taifa jijini Dar es
Salaam.
Mchezo huo ni wa kusaka nafasi ya kucheza
nusu fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC), ambapo kila mmoja
anahitaji kushinda ili aweze kusonga mbele.
Yanga
inahitaji kulipa kisasi leo, baada ya kuchapwa mabao 3-0 dhidi ya Kagera
Sugar kwenye mchezo wa ligi kuu bara msimu huu, ambapo Wana Wana
Nkurukumbi walivunja mwiko wa kutowafunga wanajangwani kwa miaka 10.
Akizungumzia
mchezo huo Meneja wa Yanga Abeid Mziba alisema, vijana wao wapo sawa
lengo lao kubwa ni kuweza kunyakua kombe la ASFC msimu huu baada ya
kulikosa taji la VPL.
“Hali ya vijana wote wapo
katika hali nzuri, timu imekamilika kiakili na kiafya wote wapo vizuri
lengo letu kubwa tumeukosa ubingwa wa ligi kuu mwaka huu akili yetu
tumeiweka kwenye ASFC.
“Kagera ni timu yenye
mwalimu na wachezaji wazuri na wachezaji wetu wapo katika hali nzuri,
nia na madhumuni yetu kufika fainali na tuchukue kombe la ASFC na safari
hiyo tunainza leo,” alisema Mziba ambaye pia ni mchezaji wa zamani wa
Yanga.
Naye Kocha wa Kagera Sugar Mecky Mexime
alisema wachezaji wao wapo vizuri japo mchezo utakuwa mgumu wamejipanga
kuondoka na ushindi na kuweza kusonga mbele.
Mchezo mwingine utakaopigwa leo, Namungo FC itawakaribisha Alliance FC ya Mwanza Uwanja wa Majaliwa Ruangwa mkoani Lindi.
KESHO
Mchezo
wa kukatana shoka utawakutanisha wababe wa soka nchini Azam FC dhidi ya
Simba SC utakaopigwa Saa 1 jioni, Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Nao Sahara All Stars itawaalika Ndanda FC ya Mtwara Uwanja wa Mkwakani jijini Tanga.
No comments:
Post a Comment