HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 08, 2020

BODI YA NAFAKA YAJIPANGA KUWA NA MASOKO YA UHAKIKA

Ofisa Masoko wa Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko Tanzania (CPB), Peter Mobe, akimuhudumia mteja katika viwanja vya maonesho ya sabasaba.
 
 Na Janeth Jovin
 

BODI ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko Tanzania (CPB), imesema imejipanga kuhakikisha kuwa na  masoko ya uhakika  kwa sababu bidhaa zao zimehakikiwa na kupata nembo ya ubora kutoka  Shirika la Viwango Tanzania (TBS).

Akizungumza kwenye viwanja vya maonesho ya 44, ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (DITF),Afisa Masoko na Mauzo wa CPB, Peter Mobe amesema mradi huo ni mkubwa unaotarajia kuanza muda wowote fedha zikipatikana na utakuwa mkombozi kwa wakulima.

Mobe amesema katika mradi huo, ghala na vihenge vyenye uwezo wa kuhifadhi mazao mchanganyiko tani 520,000 kwa mara moja litajengwa na kusaidia wakulima mbalimbali n ahata mazao ya bodi hiyo kupata eneo la kuhufadhia lililo salama.

“Hili litakuwa ghala kubwa , litakuwa mkombozi kwa wakulima na hata sisi kwa sababu pia tunanunua mazao kutoka kwa wakulima na kuyahifadhi kabla ya kuongezea thamani kwa kusaga au kukoboa ili kupata unga bora na kuuza kwa bei nzuri zaidi,amesema Mobe.

Amesema Dira ya CPB ni  kuwa taasisi yenye mtandao mkubwa katika sekta ya nafaka na mazao mchanganyiko ifikapo mwaka  2025 na kwamba karika mradi huo wa ujenzi wa ghala kubwa, vinu sita vya kusaga nafaka navyo vitajengwa.

Mobe amesema  katika ujenzi huo vinu  46  vitajengwa, maghala 36  ambayo yote kwa pamoja yatakuwa na huo uwezo wa kuhifadhi tani 520,000 kwa wakati mmoja.

“Ni kweli moja ya kazi zetu serikali iliidhinisha tufanye biashara ya nafaka na mazao nchanganyiko kama njia mojawapo ya kusaidia wakulima nchini kuwa na chombo cha uhakika kinachoweza kununua mazao yao kwa bei nzuri pia kuuza bidhaa za Tanzania zilizoongezwa thamani,”amesema Mobe.

Bidhaa zinazozalishwa na CPB ni pamoja na  unga wa mahindi sembe na dona, korosho, maharagwe, mchele,mafuta ya alizeti na mazao mengine ya nafaka.

Akizungumzia jinsi wanavyozalisha bidhaa hizo Mobe amesema wanaunua mazao bora kwa wakulima na kisha wanayachagua na kutoa uchafu wote kabla ya kupitia kwenye mashine kwa ajili ya hatua mbalimbali hadi kufikia kuzalisha unga.

“tunanunua mazao kutoka kwa wakulima na tunayachagua yale salama na safi na tolewa uchafu wote. Mfano mahindi baada ya kuyachagua yanapitishwa kwenye mashine kwenye eneo la kutoa chuma na kisha kulowekwa kwa muda maalum kutoa ganda na kutolewa alafu yanakaushwa na machine na kusagwa kutoa unga”.amesema Mobe.

Aidha CPB pia ina uza mazao hayo nje ambapo miezi miwili iliyopita waliuza mahindi tani 5,000 nchini Rwanda, pia Jamhuri ya Demokrasia ya Congo(DRC), wameuza tani 500 za unga wa mahindi na Shirika la Kimataifa la Chakula Duniani (WFP),walinunua maharage tani 5,000 na mahindi tani 6,000.

No comments:

Post a Comment

Pages