HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 04, 2020

CHUO CHA ST. JOSEPH CHABUNI TEKNOLOJIA YA KUZALISHA UMEME

Na Tatu Mohamed

CHUO cha St. Joseph Kampasi ya Dar es Salaam kimebuni teknolojia ya uzalishaji umeme kwa kutumia nguvu za miguu katika maeneo yenye watu wengi.

Akizungumza katika Maonesho ya  44 ya Biashara ya Kimataifa 'Sabasaba', mwanafunzi wa mwaka wa tatu Stashahada ya  masuala ya umeme na vifaa vyake, Denis Mrema, amesema mfumo huo unatumia mguu kukanyaga mashine baada ya hapo inachaji betri.

"Baada ya betri kuwaka inakuwa na uwezo wa kuwasha umeme na kumuwezesha mtu kuchaji simu na kuwasha taa. Teknolojia hii ilianza mwaka jana baada ya kuona inatumia gharama ndogo tuliamua kuiboresha ili kuisaidia jamii kupunguza gharama za umeme," amesema Mrema.

Ameongeza kuwa,  mfumo huo umebuniwa kwa kushirikiana na wanafunzi wenzake Josephat Chengula na Enock Samwel ambapo gharama yake inaanzia Sh. 250,000 na kuendelea kulingana na hitaji la mteja.

"Mfumo huu mbadala unaotumika zaidi kwenye maeneo ya watu wengi ambapo  hutegeshwa  maeneo yanayopita watu wengi na ukikanyaga inasaida betri kuchaji Kisha kusambaza umeme sehemu zinazohitajika, pia unaotumika zaidi maeneo ya stendi, shuleni na kwenye masomo ambapo watu wakikanyaga unazalisha umeme kwa wingi," amesema.

No comments:

Post a Comment

Pages